LATEST POSTS

Friday, March 28, 2014

Bunge lazidi kuchafuka

WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, jana wameendelea kulumbana juu ya maamuzi ya kura za wazi au za siri baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge hilo, Bw. Pandu Ameir Kificho, kuwasilisha majibu ya kamati yake juu ya kupendekeza kura ya wazi na siri, zitumike kwa pamoja.
Baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo, baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, walimtaka Mwenyekiti wa Kudumu, Bw. Samuel Sitta kumwandikia barua, Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge hilo na wajumbe wote warudi walikotoka kwani wanatumia kodi za wananchi bila kufanya kazi yoyote.
Akichangia hoja, Bw. Michael Lekule Laizer alisema Bunge hilo limechukua siku nyingi bila kupata mwafaka ikiwemo suala la kura ya siri au ya wazi huku kukiwa na mambo mengine ya msingi kama ya Serikali mbili au Serikali tatu.
Alisema ni wiki ya tatu sasa Bunge hilo limekaa lakini hakuna wanachokifanya zaidi ya kuzomea na kuwafanya wajumbe wengine kushindwa kujitokeza na kutoa msimamo wao juu ya suala hilo.
"Kama uamuzi huu wa kamati hamuutaki, basi Mwenyekiti andika barua kwa Rais alivunje Bunge turudi nyumbani kwani tunatumia kodi za wananchi na hakuna tunachokifanya.
"Katiba tunayoitaka si ya CCM wala CHADEMA, ila ni ya Watanzania wote na sijui mnagombea nini wakati Katiba ni ya wote," alisema Bw. Laizer
Naye Bi. Esther Bulaya, alisema yeye ni muumini wa kura ya siri hivyo haoni sababu ya kuanza kulumbana ikiwa kila mtu atapiga kura ya siri au ya wazi, hakutakuwa na tatizo hivyo kila mtu awe na uamuzi wake.
Bw. Joshua Nassari, alisema inashangaza kuona miaka 50 ya uhuru kuna matatizo makubwa ya maji kwa wananchi hivyo mwamuzi wa mwisho ni kura ya siri ambapo pia zimetumika katika kumchagua Mwenyekiti wa Bunge hilo na Makamu wake.
Sitta aondoka
Katika hali iliyowashtua wengi, Bw. Sitta aliomba kupumzika kutokana na udhuru alioupata na kumuachia kiti hicho Makamu wake, Bi. Samia Suluhu Hassan aendelee kuongoza Bunge hilo hali iliyowafanya wajumbe wa bunge hilo kupiga makelele.
Kwa upande wake, Bw. Mwigulu Nchemba alisema kura ya wazi ndiyo inayopaswa kutumika.
"Niwaambie wazi Watanzania wenzangu kuwa, kila mmoja ahukumiwe wazi wazi kwani Mbowe na Jussa wanataka kuleta udini na ushoga hapa...hawa ndio watu wanaotaka kukwamisha mchakato huu kwani kuna watu wanaotaka siri kwa nguvu zote ili mtegeshee wapi mtatokea,"alisema Bw. Nchemba.
Naye Bw. Felix Mkosamali, alisema inashangaza kuona watu wa makundi maalumu walioingia katika Bunge hilo wanashindwa kuwatetea wananchi ambao wakati mwingine wapinzani wamekuwa wakitoka nje kwa ajili yao

0 comments: