Hatimaye Wazazi wa mtoto Adorotea Njavike mwenye umri wa
mwaka mmoja na miezi minne wamewasili Jijini Mbeya kutoka Mkoani Njombe baada ya
kutafutwa kwa muda mrefu kutolea maelezo ya ajali ya mtoto aliyeungua moto miezi
saba iliyopita.
Ajali hiyo imepelekea ulemavu mkubwa kwa mtoto huyo
ambapo ngozi ya kidevu imeungana na kifua na kumsababishia ulemavu unaomfanya
kushindwa kula vizuri na macho kushindwa kufumba.
Baba wa mtoto huyo Joseph Njavike amesema wakati wa tukio
yeye alikuwa hayupo nyumbani kwani mtoto alibaki na mama yake mzazi aitwaye
Milika Kibelege.
Milika amesema kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa
mbili usiku alipokuwa anapika na yeye kupigwa na kitu kichwani kisha mtoto
kudondokea motoni nay eye kuzirai kabla ya mtoto kuokolewa na majirani baada ya
kusikia kilio kikali kutoka kwa mtoto.
Milika amesema
kuwa baada ya tukio mtoto alikuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji
cha Wanzali na kwamba yeye alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo hali
iliyomlazimu Dada yake kumchukua mwanae hadi Mbeya ili aweze kupatiwa matibabu
zaidi.
Kutokana na uduni wa maisha wameshindwa kufika Mbeya
kumjulia hali mtoto wao hadi walipofuatwa na Dada yake Machi 8 mwaka huu kuwa
wanahitajika Mbeya ili kibali kitolewe mtoto asafirishwe kwenda Hospitali ya
Mhimbili kwa matibabu zaidi.
Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye
alitoweka na mtoto huyo amesema anaomba radhi kwa kuondoka bila kuaga na mtoto
huyo kwani alichanganyikiwa alipoambiwa mtoto itabidi asafirishwe kwenda India
na matibabu yake yatachukua miezi sita hivyo akaona ni bora awafuate wazazi wa
mtoto huko njombe wakajadiliane
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Mbeya Thobias Mwalyego
baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waandishi wa Habari alilazimika kwenda hadi
mtaa wa Maendeleo Iyunga ili kupata maelezo ya kina kutokana na ofisi yake
kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtoto huyo.
Mwalyego amesema kuwa kuanzia sasa ataendelea kufuatilia
maendeleo ya mtoto huyo kuhakikisha anapatiwa huduma zinzostahili ukiwemo
msamaha wa matibabu kutoka Hospitali ya Rufaa
Mbeya.
Kwa upande wa wazazi wamewashukuru wasamaria wema
waliojitokeza kuchangia matibabu ya mtoto wao na madaktari wanaofanya juhudi za
kuhakikisha mtoto huyo anapatiwa upasuaji wa
haraka.
Aidha amekubali kuandamana na mwanae katika matibabu
endapo ataruhusiwa kwenda kokote na Afisa Ustawi wa Jamii alishauri pia Mama
mkubwa kuongozana na Familia hiyo kutokana na udhaifu wa mama
Adorotea
Chanzo: Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment