MTOTO Said Siraji (13), mkazi wa Majengo mjini Kahama aliyekuwa amejeruhiwa akidaiwa kuchinjwa na baba yake mzazi amefariki.
Mtoto huyo alikuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza baada ya kuchinjwa na baba yake kwa madai kuwa amechoshwa na gharama za kumtibia mara kwa mara.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia aliyekuwa akimuuguza katika Hospitali ya Bugando baada ya kuhamishwa kutoka hospitali ya Wilaya ya Kahama, Hussein Idd, mtoto huyo alifariki juzi saa 2 asubuhi.
Idd alisema mtoto huyo alikuwa akisoma darasa la tatu katika shule ya msingi Majengo mjini Kahama alifanyiwa unyama huo na baba yake mzazi, (jina linahifadhiwa).
Alidai baada ya kuchinjwa wasamaria wema walimwokoa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Kahama, ambako alilazwa kwa matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya, alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambako mauti yamemkuta.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo, Noely Mseveni, alisema mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwa mama yake mzazi, Mariamu Idd.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dkt. Joseph Fwoma, alisema mtoto alihamishiwa Bugando kwa matibabu kutokana na kujeruhiwa vibaya.
Uongozi wa Hospitali ya Bugando wamethibitisha kifo cha mtoto huyo.

0 comments:
Post a Comment