LATEST POSTS

Monday, April 14, 2014

HATIMAYE ASHA BARAKA AOLEWA



WERAWERAAA! Baada ya kuishi kwa muda mrefu tangu alipotengana na mumewe Khamis Bwela, Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka ‘Iron Lady’ usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita alifunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Dar aitwaye Idd Baka Pandisha, Ijumaa Wikienda lina mzigo kamili.

Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka ‘Iron Lady akifunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Dar aitwaye Idd Baka Pandisha usiku wa kuamkia ijumaa iliyopita.

Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo ya Magomeni-Usalama, Dar, nyumbani kwa mkurugenzi huyo ambapo watu wachache ndiyo waliohudhuria huku mdogo wa bi harusi, mama yake Nasibu Abdul ‘Diamond’ Sanura Kasim a.k.a Sandra  akiwa ndiye msimamizi wa shughuli nzima.
“Yaani ukaribu wote huo na Asha Baraka hamjaalikwa (Global)? Basi kwa taarifa yenu amefunga ndoa ya siri ili kujiweka sawa katika pilika zake za kugombea ubunge,” alisema mtonyaji wetu aliyekuwa ndani ya nyumba.
Baada ya kupata ‘niuzi’ hizo motomoto, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Asha Baraka ili kutaka kujua furaha yake ikoje baada ya kufunga ndoa ambapo bila kutegemea paparazi alikumbana na sauti ya maombi ya kwamba asitiriwe.
“Ni kweli nimefunga ndoa lakini naombeni mnisitiri kwani mtaniharibia kila kitu, chondechonde jamani mimi ni mtu wenu pia ni  kama dada yenu,” alisema Asha Baraka. Kwa muda mrefu Asha Baraka amekuwa mwenyewe bila mume baada ya kutengana na Bwela ambaye alimuoa mwigizaji Tamrina Poshi ‘Amanda’ waliyetengana hivi karibuni.

0 comments: