LATEST POSTS

Sunday, April 13, 2014

MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA

 
Maalim Muhidin Gurumo enzi za uhai wake.

MKONGWE wa Dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo aliyekuwa akitumikia Bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ kabla ya kustaafu mwaka jana, amefariki  dunia.
Kwa mujibu wa habari tulizozipata kupitia chanzo chetu, Mwanamuziki huyo amefariki alasiri hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mpaka sasa sababu ya kifo cha Mzee Gurumo bado haijajulikana na taratibu za mazishi bado hajizafahamika.

0 comments: