WAZIRI wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ameakiahidi chuo cha
Musoma Utalii kilichpo mkoani Tabora ataleta watalaamu wa mafunzo ya
utalii na uzuiaji majangili.
Ahadi hiyo aliitoa kwenye mahafali ya kumi ya chuo hicho,pia baada ya
uzinduzi wa chuo hicho kilichopo Ipuli manispaa Tabora.
Nyalandu alisema ipo haja ya kuleta watalaam hao chuoni hapo ili
mafunzo yatakayotolewa yawe chachu kwa siku zijazo katika vita ya
ujangili nchini.
Aidha waziri huyo aliwataka wahitimu hao 165 kutumia mafunzo
waliyopata kubadili maisha yao na taifa kwa ujumla.
Alifafanua kuwa wahitimu wanatakiwa kuwa na imani kutumia ujuzi
walioupa kwani jamii iliyostarabika siku zote imani inapokuwepo hakuna
kinachoshindikana.
"Ndugu zangu wahitimu mnapaswa kutambua siku zote riziki inatafutwa
hivyo make tayari kutafuta riziki hiyo kwa mafunzo mliyopata kwa
kuisadia jamii na taifa kwa ujumla."aliongeza.
Hata hivyo aliwaomba wahitimu hao kujitoa kama vijana kulitumikia
taifa hili kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumethubutukuelekea
mafanikio.
Alisema iko haja kwa vijana kuandaliwa ili kuja kuleta mabadiliko
tarajiwa na kufikiwa kwa malengo ya 'Big Result Now'.
Aidha waziri huyo aliwaomba ahitimu hao kuwa na utayari wa kuchukia
matendo ya ujangili yanaoendelea na kuomba wawe tayari kujitoa kwa
ajili ya nchi yao kwenye vita hiyo.
LATEST POSTS
Wednesday, April 9, 2014
Home »
» NYALANDU AAHIDI NEEMA MUSOMA UTALII TABORA.
0 comments:
Post a Comment