Kanisa la Ntarama, ambako wakimbizi elfu tano kutoka
jamii ya watutsi waliyouawa aprili 15 mwaka 1994.
jamii ya watutsi waliyouawa aprili 15 mwaka 1994.
RFI/N.Champeaux
Wananchi wa Rwanda wameadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 tangu
kutokea kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliosababisha vifo vya
watu laki nane kwa kipindi cha siku mia moja. Maadhimisho hayo
yamefanyika jijini Kigali na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka
Barani Afrika na wawakilishi wa mataifa ya magharibi pamoja na katibu
mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ambaye amesema Jumuiya ya kimataifa
bado inajuta kwa kutozuia mauaji hayo.
Katika hotuba yake rais Paul Kagame amesisitiza kuwa Historia
ya mauaji hayo ya kimbari hayawezi kufutika na kuyataka baadhi ya
mataifa kama Ufaransa kukiri wazi kuwa ilishiriki katika mauaji hayo.
Katika hatua nyingine, ujumbe wa Ufaransa uliotarajiwa kuwasili
nchini Rwanda kushiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ishirini
tangu mauaji ya kimbari yatokee nchini humo umeamua kutoshiriki.
Hata balozi wa Ufaransa mjini Kigali, ambae alitakiwa kuliwakilisha
taifa lake, amefahamisha kwamba hatoshiriki katika sherehe hizo,
akibaini kwamba hakupata kibali maalumu kinachotolewa na itifaki ya
Rwanda kwa viongozi wanaohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya
mauaji ya kimbari.
Christiane Taubira, waziri wa sheria wa Ufaransa.
Reuters/Charles Platiau
Waziri
wa sheria wa Ufaransa Christiane Taubira alitarajiwa kuongoza ujumbe
huo, lakini hatua ya kusitisha ushiriki wa nchi hiyo unatokana na
matamshi ya viongozi wa Rwanda kuendelea kuituhumu Ufaransa kuhusika kwa
njia moja au nyingine kwa kile kilichotokea nchini Rwanda mwaka 1994,
wakati Ufaransa ilikua iliwatuma wanajeshi wake kuwalindia usalama raia
katika maeneo yaliyokua yalitengwa, ambayo yalijulikana kwa jina la
“zone turquoise”.
Kauli hiyo ya rais Kagame haikutofautiana na ya waziri wake wa mambo
ya ndani Louise Mushikiwabo ambaye amekosoa hatua ya serikali ya
Ufanaransa kusitisha ushiriki wao kwenye sherehe hizo na kusema kuwa
licha ya hayo, bado historia ina nafasi yake.
Katika hatua nyingine, rais Kagame amegusia mahusiano ya nchi yake na baadhi ya nchi nyingine ikiwemo Afrika Kusini
ambayo imeghadhabishwa na ushiriki wa baadhi ya wanadiplomasia wa
Rwanda katika jaribio la kumuua Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, na
kubainisha kuwa bado nchi yake inahitaji uhusiano mzuri na Afrika kusini
kwa vile bado tuhuma hizo hajizathibitishwa.
Rais Kagame aliongoza sherehe hizo kwenye uwanja wa mpira wa Amahoro,
ambapo wakiwepo baadhi ya marais na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban
Ki Moon, huku nchi ya Burundi nayo ikiazimisha kumbukumbu ya miaka
ishirini ya rais wao Cyprien Ntaryamira ambaye aliuawa kwenye ndege
pamoja na rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana.
Chanzo:RFI Kiswahili
0 comments:
Post a Comment