LATEST POSTS

Monday, April 21, 2014

WATU 10 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA BASI KUGONGA NYUMBA NA KUPINDUKA MKOANI SIMIYU



 
WATU 10 wamekufa  papo hapo mmoja kufariki akiwa hospitali  na wengine 30 kujeruhiwa vibaya kufuatia
ajali mbaya ya Basi la Luhuye Express lililokuwa likitoka wilayani
Tarime mkoani Mara kuelekea Jijini Mwanza.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa  kwa njia ya simu na Kamanda wa
Polisi mkoa wa Simiyu,Kamishina Mwandamizi wa Polisi(SACP)Charles
Mkumbo zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:11 asubuhi
katika kijiji cha Itwimila wilayani Busega.
 
Alisema kuwa basi hilo lenye namba za usajili T 410 AWT liliacha njia
na  kugonga nyumba  ya Marehemu , Mwalimu Lazaro Mbofu  na kuibomoa
yote na kisha kupinduka .
 
Kamanda Mkumbo alisema hadi sasa wametoa miili ya watu 10 katika basi
hilo na majeruhi zaidi 30 wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando kwa matibabu zaidi.
 
“Hadi sasa kuna maiti 10 zilizopatikana eneo la tukio na zaidi ya watu
30 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Bugando kwa ajili ya
matibabu ila taarifa kamili nitaitoa baadaye juu ya watu waliokufa na
waliojeruhiwa kwani sasa nimetuma askari wa usalama barabarani
kufuatilia”alisema.
 
Mmoja wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo,Juma Ally mkazi wa kijiji
cha Itwimila akiongea na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa
aliona basi hilo likiwa kasi na kupoteza mwelekeo na kutoka barabarani
na kisha kuigonga nyumba hiyo  na kuipita juu ya paa na kupinduka.
 
“niliona Basi hilo lililokuwa likitokea barabara ya Musoma kuelekea
Mwanza likiwa katika mwendo wa kasi na dereva nadhani alishindwa
kulimudu na kisha kutoka nje ya barabara na kuigonga nyumba na kisha
likapita juu ya nyumba hiyo na  kupinduka”alisema.

0 comments: