LATEST POSTS

Thursday, May 1, 2014

MATESO MAKALI;KIJANA AOTA MAGAMBA AOTA MAGAMBA YA MTI BAADA

 
 
 
                                                                 








Stori: Andrew Carlos na Nyemo Chilongani
AMA KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA! Kijana, Andrea John, 26, amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kupatwa na ugonjwa wa ajabu uliosababisha mguu wake kuwa na magamba mithili ya mti mkavu
CHANZO CHA UGONJWA Andrea anayeishi kwa mateso makali maeneo ya Argentina, Manzese jijini Dar, anasema mwaka 2005 akiwa anafanya kazi katika mashine ya kusaga na kukoboa, alijikuta akianza kuumwa na vidole vya mguu wa kulia na baadaye maumivu hayo kuhamia kiunoni, kitu kilichomfanya kukosa raha.
Anaendelea kusimulia: “Mara baada ya kusikia maumivu ya vidole na kiuno, nilikwenda katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Nilipofika huko, wakaamua kuchukua vipimo vya damu kwa ajili ya uchunguzi lakini hawakutaka kunipa majibu, nilishangaza sana kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho.
 KUFIWA NA MKE
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Kutokana na matatizo ya kuugua nilishindwa kumlea mtoto wangu hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nafanya kazi, bahati nzuri mwanamke mmoja wa Kiarabu alijitokeza na kuamua kumchukua Agness na kuishi naye,” alisema Andrea kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa aliendelea kupata matibabu japokuwa hayakubadilisha kitu chochote zaidi ya mguu wake kuanza kuota magamba ambayo yaliufanya kubadilika na kufanana na mti uliokauka. Baada ya kuona hali imekuwa hivyo na maumivu yakimzidia kila siku, aliamua kurudi Hospitali ya Mwananyamala ambapo walimwambia achukuliwe vipimo kwa mara nyingine.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
“Kilichofanyika ni kuchukuliwa vipimo kwa kutumia kipimo cha kupimia saratani ya ngozi ambacho hujulikana kitaalamu kama Biopsy na hivyo kukutwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi uitwao Kaposis Sarcoma,” alisema.
Alisema hakuweza kupatiwa matibabu zaidi ya kuandikiwa karatasi ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar.
Alipokuwa Muhimbili, Andrea alilazwa kwa muda wa miezi miwili bure kutokana na kutokuwa na uwezo kifedha, madaktari waliliangalia tatizo lake kiundani na wakashauri asikatwe mguu hivyo wakamuandikia dozi ya dawa za vidonge na kumruhusu kurudi nyumbani.
Mpaka sasa Andrea anaendelea na vidonge hivyo na hana msaada wowote zaidi ya kutembea mtaani na kuomba chochote japo apate chakula cha siku na anashindwa kurudi hospitali kwa kuwa hana hata senti tano.
Andrea anaomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na habari hii ili aweze kupata fedha za kuendeleza matibabu yake na kujikimu. Kutoa ni moyo na ukimsaidia utapata baraka za Mungu. Unaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya dada yake.

   
 

0 comments: