MBUNGE waviti maalumu mkoa wa Mara kupitia vijana Ester
Bulaya(CCM) ametoa msaada wa mashuka 200 kwenye kituo cha afya cha
Manyamanyama kilichopo wilayani Bunda ikiwa ni jitihada za kuchangia
kituo hicho kilicho kwenye mchakato wa kutangazwa hospitali ya Wilaya.
Akikabidhi msaada huo kwa wagonjwa waliokuwa
wamelazwa kwenye wodi ya Wanawake,Watoto naWanaume,Bulaya alisema akiwa
kama mkazi wa Manyamanyama,Bunda na kiongozi anayeguswa namasuala ya
kijamii aliguswa na uhaba wa mashuka kwenye kituo hicho na kuamua
kuchangia sehemu ya upungufu.
Alisema alipotembelea kituo hicho kwa siku za nyuma alipewa taarifa ya upungufu mkubwa wa mashuka
kwenye kituo hicho na kupelekea wagonjwa kulala bila kijifuni wala
kutandika na kuamua kujibana katika sehemu ya kipato chake na kununua
mashuka 200 kwa kuanzia.
Mbunge huyo ambaye mara kadhaa amekuwa
akizungumzia kituo hicho cha afya bungeni na namna ambavyo licha ya
kuhudumia wangonjwa wengi kutokana na kuwa jirani na barabara kuu
kuiomba Serikali kukamilisha mapema mchakato wa kuitangaza kuwa
hospitali ya Wilaya ili iweze kupata mahitaji stahiki na kuwahudumia
wagonjwa wanaofika kwenye kituo hicho.
Alisema mashuka hayo 200 aliyotoa kwa namna
moja yatasaidia kupunguza changamoto ya wagonjwa kupatwa na baridi na
hata kutandika kwenye vitanda na pale atakapopata nafasi ataendelea
kuchangia mahitaji mbalimbali yanayohitaji kakwenye kituo hicho ikiwa ni
pamoja na vifaa tiba,madawa na kubwa ni kuhakikisha unazungushwa uzio
ili kuzuia watu kuvamia maeneo ya hospitali.
Kutoka na namchakato wa kupandishwa hadhi
kituo hicho na kuwa hospitali ya Wilaya,Bulaya aliiomba Serikali kufanya
jitihada za makusudi kukipa hadhi kituo hicho na kuwa hospitali
kutokana na kutoa huduma muhimu licha ya changamoto ambazo zipo kwenye
kituo.
Akizungumzia
msaada uliotolewa na Ester Bulaya,Mganga wa Wilaya ya Bunda Charles
Mkombe alisema msaada alioutoa mbunge huyo umekuja wakati muafaka ambapo
kituo hicho cha afya kinakabiliwa na uhaba wa mashuka 640 ili kukidhi
haja.
Alisema msaada huo umepunguz upungufu mkubwa
uliokuwepo na kumshukuru Mbunge huyo kwa kuwa na moyo wakujali mahitaji
hususani ya wagonjwa wanaofika na kulazwa kwenye kituo hicho cha afya
ambacho kinatumiwa na watu wengi.
Mkombe
alisema mashuka ni moja ya changamoto kubwa waliokuwa nayo licha ya
kuwepo na changamoto nyingine ikiwemo kutukuwa na uzio wa kuzunguka
kituo hicho cha Manyamanyama na kupelekea baadhi ya watu kuvamia maeneo
ya hospitali na kushukuru kauli ya Bulaya kuonyesha utayari wa kusaidia
kuzungushwa uzio huo.
Baadhi
ya wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye wodi na kupokea msaada wamashuka
hayo,walimshukuru Mbunge huyo kwa kuwa walikuwa wakipata tabu sana
hususani nyakati za usiku kwa kushikwa na baridi kutokana na kukosa
mashuka ya kujifunika.
0 comments:
Post a Comment