LATEST POSTS

Wednesday, July 9, 2014

MTOTO WA MIAKA 9 AVUNJA REKODI YA KUFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Mtoto Idda Baita (9), akiinua mikono juu kwa furaha baada ya kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro
.
MTOTO Idda Baita ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Uwanja wa Ndege Moshi, amevunja rekodi ya kuwa mtoto wa kwanza wa kike kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro chenye urefu wa Mita 5739.
Idda alitumia njia ya Umbwe, Kibosho njia inayosemekana kuwa ni ngumu hata kwa watu wazima  kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Idda amesema atakuwa balozi mzuri wa Kilimanjaro National Park kwa watalii wanaokuja Tanzania kwa madhumuni ya kupanda mlima huo.

0 comments: