Akizungumza kwenye Mahafali ya Chuo cha Uuguzi cha Masista wa Kanisa
Katoliki Kanosa Mugana, Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera jana, Sitta
alisema wengi wa waliotangaza nia hawafai na kwamba wanapiga porojo tu.
Mjadala wa urais mwaka 2015 unaonekana kuanza kuitikisa nchi
kutokana na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kujitokeza
hadharani na kutangaza nia, huku wasomi, viongozi wa dini, wanaharakati
na vyama vya siasa wakitaja sifa za mgombea.
Mmoja wa vigogo hao wa CCM ni Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye jana alijitokeza na
kusema atajitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais iwapo wataendelea
kujitokeza wasiokuwa na sifa.
Akizungumza kwenye Mahafali ya Chuo cha Uuguzi cha
Masista wa Kanisa Katoliki Kanosa Mugana, Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa
Kagera jana, Sitta alisema wengi wa waliotangaza nia hawafai na kwamba
wanapiga porojo tu.
Sitta alisema wengine wamejitokeza kwa ‘gia’ ya
ajira, lakini hawabainishi chanzo chake, kwani tatizo hilo limetokana na
ufisadi kwa baadhi ya viongozi.
Aliwataka wananchi kuwapima wagombea kwa makini
kwani wapo baadhi yao wanajinadi kuwa wao ni vijana kitu ambacho siyo
kigezo cha kuwa rais.
“Ndugu zangu Watanzania, tusipowachuja watu kwa
chujio la tabia zao, tutaangukia mtego wa kuwapima watu kama vile
tunafanya mzaha, maana kuna wengine wameanza kusema nichagueni mimi ni
kijana, hivi kwani urais ni mashindano ya ulimbwende, tunatafuta mzuri?”
alihoji.
Awaponda waliotangaza nia
Alisema akiangalia orodha ya waliojitokeza haifai na kwamba, labda watu kama wawili wanaoweza kuungwa mkono lakini hakuwataja.
Waziri Sitta alitumia hadhara hiyo kuihadharisha
jamii kuona suala la uchaguzi wa rais kama jambo la kawaida, kwani
ikicheza nchi itazama.
”Niseme jingine, kwa kuwa nikitazama hiyo anga ya
hawa wanaotafuta ukubwa, nawaona kama mmoja wawili ndiyo kidogo unaweza
kuwaunga mkono. Hali hii ikiendelea namna hii, eeh itabidi na sisi wazee
tujitose manake ikiwa watu wenyewe hawa ni walaghai, wengine ni waongo,
wengine rekodi mbaya, wengine walishiriki kuhujumu nchi, ndiyo
wanakwenda kimbelembele wanapigana vikumbo.
Wasomi, wanaharakati
Wakati Sitta akisema hayo, wasomi, wanasiasa na
wanaharakati wamesema rais ajaye anatakiwa kuwa mzalendo, msomi,
mwadilifu, mchapakazi, anayejua matatizo ya nchi na wananchi na akubali
kuyatatua, asiwe mbaguzi, mwenye uamuzi mgumu, anayetanguliza masilahi
ya taifa mbele na atakayepambana na rushwa na ufisadi kwa vitendo.
Kauli za wadau hao zimekuja kipindi ambacho watu wa kada
mbalimbali, hasa kutoka ndani CCM wakiweka wazi nia zao za kugombea
urais mwaka 2015, kufikia hatua ya chama hicho kuwapa adhabu makada wake
sita, kutokana na kuanza kampeni mapema.
Makada waliopewa adhabu ya mwaka mmoja kwa tuhuma
za kuanza kampeni za kuwania urais kabla ya wakati ni January Makamba,
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick
Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe. Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu)
Steven Wassira pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini
ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Makamba takribani siku nane zilizopita akiwa
jijini London, Uingereza, alitangaza nia yake ya kuwania urais mwaka
2015, akisema huu ni wakati wa fikra mpya ambazo zinahitaji vijana na
kwamba wazee wakae kando.
Hata hivyo, Makamba alipingwa na Rais Jakaya
Kikwete ambaye alisema kuwa naibu waziri huyo anataka mambo makubwa,
kwamba, “asilazimishe” kwa kuwa wakati ukifika atapata kile
anachokitaka. Alhamisi iliyopita Sumaye akiwa mkoani Mwanza alinukuliwa
na vyombo mbalimbali vya habari, akisema kuwa ana nia ya kugombea urais,
lakini mpaka atakapoombwa kufanya hivyo.
Januari mosi mwaka huu, licha ya kutokuweka wazi
Lowassa alitangaza kuanza rasmi kwa safari aliyoiita ya matumaini ya
ndoto zake, ambayo amesema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu
bure, majisafi na maendeleo ya uhakika.
Hata hivyo, makada hao huenda wakakumbwa na rungu
jingine baada ya siku tatu zilizopita chama hicho kutoa maagizo kwa
Kamati yake ya Usalama na Maadili kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa
adhabu kwa vigogo hao waliotangaza nia kabla ya wakati.
Wasomi
Profesa wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, George Shumbusho
alisema nchi ilipofikia inahitaji rais mwadilifu atakayekuwa tayari
kuchukua uamuzi mgumu bila woga kwa viongozi wote ambao hawatakuwa
waadilifu.
“Umri siyo hoja wala taabu, tunataka rais
anayethubutu kutenda haki na mwenye kuzingatia maadili, kuwaunganisha
Watanzania wote, lakini aweze kuchukua hatua kwa wasio waadilifu hata
kama ni ndugu, jamaa au rafiki yake.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,
Profesa Tolly Mbwete alisema, rais ajaye anatakiwa awe mwelewa wa kiasi
kikubwa hasa katika masuala ya uchumi na mwenye muono wa Tanzania mpya
alipoikuta na anakotaka kuifikisha.
Wanaharakati
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema nchi ilivyo sasa suala
la umri isiwe sababu, kwani mtu yeyote anaweza kuwa rais.
Alisema rais ni lazima awe mtu mwenye upeo mkubwa wa kupokea mabadiliko yatakayojitokeza na kuyafanyia kazi.
“Ujana haunipi shida, lakini ana uwezo? Kuna
vijana wako makini kutuongoza, hivyo tusiwanyime nafasi kwa umri wao.
Tuangalie ni jinsi gani atatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
nchi,” alisema Dk Bisimba.
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP), Ussu Mallya alisema, “Kiongozi tunayemtaka awe
anaelewa na awe na msimamo thabiti wa kuendeleza nchi bila kujali kuwa
ni mwanamke, kijana, mwanaume au mzee.” Aliongeza; “Tunahitaji kumpata
kiongozi atakayepambana na rushwa, uzembe na kipindi hiki mtu wa aina
hii ndiyo tunayemtaka.”
Vyama vya Siasa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha),
John Heche alisema umri, jinsia na rangi haijawahi kuwa sifa ya urais
hiyo ni kampeni ya kibaguzi.
Alisema rais anayehitajika ni yule anayejua
matatizo ya wananchi, atakayeitoa nchi iliyo katika matumaini
yaliyofifia kwenda mbele zaidi.
Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mosena
Nyambabe alitaja sifa nne za rais ajaye na kufafanua kuwa umri ni kigezo
cha kibaguzi.
“Rais lazima awe mzalendo, mwenye maadili,
anayejua matatizo ya nchi yake na Watanzania na awe na majibu yake na
asimamie misingi ya utawala bora iliyoanza kupotea na kuhakikisha kuwa
anapambana na rushwa na ufisadi,” alisema.
Viongozi wa dini
Wakizungumza na gazeti hili Askofu Furaha
Mwambusye wa Kanisa la Haven of Peace, Ammy Mwakitalu wa Kanisa la
TAG-Tabata, David Samson (Jesus Power-Musoma) na Boniphati Makasi
(EAGT-Bunju) na Askofu Mkuu wa Kanisa la Power Miracle, Joachim Peter
walitaja sifa nne za anayefaa kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Askofu Peter
alitaja sifa ya kwanza kuwa ni kiongozi mwenye kumcha Mungu, ambaye
hatakuwa tayari kufanya jambo bila kumshirikisha Mungu.
“Taifa letu halihitaji viongozi wenye tuhuma za rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka,” alisema Peter.

Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment