Tumekwisha! Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata
ambao si riziki (mashoga) na wanawake wanaojishughulisha na mapenzi ya
jinsi moja (wasagaji) kutoka nchi mbalimbali wamefanya mkutano wao
mkubwa wa kimataifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.
Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa
nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na
wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.
Baada ya kupata taarifa hizo, kachero wa Ijumaa Wikienda alizama
ndani kimafia ambapo alinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa
ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini.
Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
0 comments:
Post a Comment