Wabunge watano wamepewa
adhabu ya kutokuhudhuria vikao vya mkutano wa 20 wa bunge, kwa madai ya
kukiuka kanuni za bunge na kusababisha vurugu hali iliyopelekea spika wa
bunge kuahirisha bunge.
Adhabu hiyo imetolewa na
kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge ambapo waliosimamishwa ni Mh
Tundu Lissu, Mh John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekul na Mh Felix
Mkosamali ambao hawataweza kuhudhuria vikao vya bunge hili hadi
litakapovunjwa na wabunge wengine wawili Mh Peter Msigwa na Mh Rajab
Mbarouck Mohamed wamezuiliwa kuingia vikao viwili vya bunge ambapo
akisoma maamuzi hayo mjumbe wa kamati hiyo Mh Hassan Ngwilizi amesema.
Vurugu hizo zilitokea
wakati waziri wa nishati na madini Mh Simba Chawene akiwasilisha muswada
wa sheria ya petroli bungeni mjini Dodoma ambapo wabunge wa upinzani
walianza kuomba muongozo wa spika huku Mh Chawene akiendelea kusoma
muswada huo lakini baada ya muda alishindwa kuendelea baada ya kuzidiwa
na kelele za wabunge hao hali iliyosababisha spika wa bunge Mh Anne
Makinda kuahirisha bunge.
Mara baada ya kikao cha
bunge kuahirishwa nje ya ukumbi wa bunge mbunge wa Ubungo Mh John Mnyika
akazungumzia suala hilo kwa niaba ya wabunge wa kambi ya upinzani
bungeni ambapo amesema kambi ya upinzania haiko tayari kuua ndoto za
watanzania za kuondokana na umaskini kwa kutumia rasilimali zao na hapa
anafafanua zaidi sababu za wao kupinga miswada hiyo.
Waziri wa nchi, ofisi ya
waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh Jenista Mhagama amekanusha madai
ya miswada hiyo kujadiliwa kwa siku moja na kudai kuwa ingeweza
kujadiliwa hadi pale ambapo wabunge wangefikia muafaka na kuongeza kuwa
ndiyo maana serikali iliamua isomwe mwishoni baada ya miswada mingine
yote kujadiliwa.
0 comments:
Post a Comment