Duniani kuna mambo mengi ya ajabu ambayo umewahi au hujawahi kusikia.
Gazeti hili linapanda milima na kushuka mabondeni kisha kupaa angani
kukuletea simulizi ya undani wa viumbe wa ajabu waishio au waonekanao
angani. Ungana nami katika simulizi hii.
Huko nyuma niliwahi kudokeza kwenye gazeti tumbo moja na hili, Ijumaa
Wikienda lakini sikuingia ndani ili kupata ukweli juu ya viumbe hao wa
ajabu waishio angani. Wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu
isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao
waliogundulika karne kadhaa zilizopita, wameshatengenezewa filamu nyingi
na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).
Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.
Inaaminika kuwa, Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo! Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Wachambuzi wa mambo ya anga walishaandika ripoti nyingi kuhusu viumbe hao ambao huja duniani na kurudi angani.
Swali ni je, viumbe hao wanaishi katika sayari gani? Wataalam hao wanalijibu swali hilo kwa kusema haijulikani moja kwa moja wanaishi sayari gani lakini kwa uhakika siyo kwenye mwezi (kumbuka mwezi siyo sayari).

Inawezekana bado hujaelewa simulizi hii. Bermuda Triangle ni eneo la
pembetatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika Bahari ya
Atlantiki. Miaka kadhaa huko nyuma viumbe hao waliwahi kutua eneo hilo
na kuweka historia (nitaisimulia huko mbele). Pia waliwahi kuonekana
Kisiwa cha Bermuda, Pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto
Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida,
Marekani.
Umewahi kusikia vitu mbalimbali duniani vikisemekana vimepotea katika
mazingira ya kutatanisha? Aliens wanahusishwa na upoteaji wa meli
baharini hasa za mizigo huku watu wakiamini huwa zinazama lakini
uchunguzi ukifanyika meli hizo huwa hazionekani hata ndani ya maji
baharini.
Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa
labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe
hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana
milele katika eneo la Bermuda Triangle ikieleza kuwa Aliens ndiyo
wahusika wa upotevu huo.
Ujio wa Aliens katika eneo la Bermuda Triangle ulisababisha kisiwa
hicho kupata umaarufu duniani na kupewa jina la Devil’s Sea (Bahari ya
Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu kuwa
shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa
majini. Wengine huhisi ni ushirikina.
Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Wataalam wa anga wanadai Aliens wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.
>> Je, hawa ni viumbe gani? Ndiyo kwanza simulizi imeanza. Usikose kufuatilia wiki ijayo.
>> Je, hawa ni viumbe gani? Ndiyo kwanza simulizi imeanza. Usikose kufuatilia wiki ijayo.
Chanzo: Global Publishers
0 comments:
Post a Comment