LAZIMA wakae! Ndivyo unavyoweza kusema
kufuatia umati mkubwa kujitokeza kumsindikiza mgombea urais wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), John Pombe Magufuli (pichani)kwenda kuchukua fomu ya
urais Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Posta-Mpya, jijini Dar,
Amani linakupa mchapo kamili.
Juzi, Magufuli (pichani) akiambatana na
mgombea mwenza, Samia Suluhu wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bara, Phillip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana walianza
msafara kuanzia kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba
kuelekea makao makuu hayo ya NEC kuchukua fomu hiyo.Wakizungumzia
msafara huo uliosimamisha shughuli zote kwa muda, baadhi ya wakazi wa
Jiji la Dar walisema kutokana na muitikio mkubwa wa wanachama na wasio
wanachama waliojitokeza, ni dhahiri itakapofika siku ya uchaguzi, Oktoba
25, mwaka huu, wapinzani lazima wakae kwani Magufuli ni jembe.
“Lazima wakae wapinzani, tena na hivi
wanavyoanza kugawanyika mara sijui katibu mkuu wao Slaa amejiengua
hawaiwezi CCM hata kidogo.
Mwenyekiti wa CCM taifa, Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza makao makuu ya CCM taifa jijini Dar, wakati wa uchuaji fomu hizo.
“Magufuli ni msafi, hana doa hata moja.
Utendaji wake wa kazi umetukuka. Kila Mtanzania anajua namna ambavyo
amekuwa akisimamia sheria katika ujenzi wa barabara, kupushi mambo
yaende kwenye mstari na hata kuwafokea hadharani watumishi wanaozembea
kazini,” alisema Kery Masabwite mmoja wa wakazi wa Dar na kuongeza:
Umati wa watu waliofurika kushuhudia Magufuli akichukua fomu ya kuwania urais.
“Watu wengi ambao si wanachama wa CCM
wameguswa sana uteuzi wa Magufuli. Kama hiyo haitoshi, kuna wafuasi wa
Chadema na Ukawa ambao hawakufurahishwa na Edward Lowassa kuingia kwenye
chama chao, wote wamekihama na watapigia kura CCM.”
Akizungumza katika mkutano wa hadhara
katika ofisi hizo ndogo za CCM mara baada ya Magufuli kuchukua fomu,
Rais Jakaya Kikwete alisema tukio hilo lilikuwa muhimu kwake hivyo
isingekuwa rahisi kutokuwepo.
“Kuchukua fomu kwa wagombea wetu ni moja
ya shughuli muhimu katika chama ndiyo maana niko hapa leo, najivunia
pia juzi kuwepo Australia, walinipongeza kwa kuongoza kwa demokrasia na
kuwapa watu uhuru wa kuchagua chama wakitakacho. Watanzania wajiandae
kwa uzinduzi rasmi wa kampeni tutakaoufanya Agosti 22, mwaka huu,”
alisema Kikwete.
Mbali na Kikwete, shughuli hiyo
ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM kuanzia wilaya hadi taifa
akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
0 comments:
Post a Comment