Mtayarishaji wa vipindi, Sospiter Jonas
amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma Mjini akishtakiwa kwa
matumizi mabaya ya mtandao.
Sospiter alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mussa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Emmanuel Bwile.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook ujumbe kuwa “Pinda utakuwa muhubiri wa injili tu.”
Mussa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa
huyo alibandika picha ya John Maliga kwenye ukurasa wake wa Facebook na
kuandika ujumbe huo, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu namba 16
cha Sheria ya Mtandao ya Mwaka 2015.
Mlalamikaji katika shauri hilo la jinai namba 815/2015 litakalokuja tena mahakamani Oktoba 19, ni John Maliga.
Mshtakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya Sh1 milioni.
Kesi hii imekuja baada ya wiki
iliyopita, kijana mmoja, Benedict Ngonyani (24) kufikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza
taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis
Mwamunyange.
Kijana huyo anatuhumiwa kuandika katika
ukurasa wake wa Facebook na WhatsApp kuwa, Mwamunyange, amelazwa kwenye
hospitali moja mjini Nairobi, Kenya kwa madai ya kulishwa chakula
chenye sumu
0 comments:
Post a Comment