Lamar Odom.
MUNGU mkubwa! Lamar Odom mwishoni mwa wiki hii aliamka baada ya kupoteza fahamu kwa zaidi ya siku tatu, kwa madai ya kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya, lakini Ijumaa iliyopita alizinduka baada ya kusikia sauti ya mkewe, Khloe Kardashian, akimwambia ‘I love you’.
Lamar,
35, ambaye ni staa wa zamani wa NBA, aliripotiwa kupoteza fahamu tangu
Oktoba 13, mwaka huu na kulazwa kwenye Hospitali ya Sunrise huko Las
Vegas huku aliyekuwa mkewe, Khloe akionekana kuwa naye karibu sana.
Hata hivyo, Khloe ambaye alikuwa akifuatilia talaka mahakamani ili
aachane na Lamar, ameonekana kusitisha ili aweze kuwa karibu zaidi na
mumewe huyo wa ndoa kwa kipindi hiki kigumu.Lamar ana watoto wawili
ambao alizaa na aliyekuwa mpenzi wake, Liza Morales, ambao ni Destiny,
17 na Lamar Odom Jr, 13.
0 comments:
Post a Comment