LATEST POSTS

Saturday, November 7, 2015

MAGUFULI AFUTA SAFARI ZOTE ZA NJE YA NCHI KUANZIA LEO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli.

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo maamuzi mengine yatakapotolewa.
Dk Magufuli ameagiza shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa  na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje.
Uamuzi huo wa rais ameutoa Ikulu jijini Dar es Salaam katika   kikao kilichojumuisha watendaji mbalimbali wa serikali wakiwemo Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari ruhusa ya safari nje ya nchi inaweza kutolewa kwa jambo la dharura ambalo hata hivyo jambo hilo lazima lipate kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
“Badala yake rais ametaka ziara nyingi zielekezwe kwenda vijijini ili kuwawezesha watendaji kujua na kutatua kero za wananchi” imesema taarifa hiyo.
Katika kikao hicho, rais ameelekeza pia mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili yasimamiwe mara moja na Baraza la Mawaziri atakaloliteua.
Mambo hayo ni pamoja na kuanza kwa mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wote wanaanza kupatiwa elimu ya bure kuanzia Januari mwakani.
Taarifa hiyo imetaja jambo la pili kuwa ni suala la uratibu wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo ameagiza lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, rais amemuagiza Kamishna wa TRA kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kero ndogo ndogo zinazowakabili wananchi zinaanza kushughulikiwa mara moja.
Ameitaka TRA kukusanya mapato toka kwa wafanya biashara wakubwa na wakwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote na kusisitiza kuwa hakuna mwenye mamlaka ya kubatilisha maamuzi hayo zaidi yake.

Chanzo: Global publishers

Saturday, October 31, 2015

Friday, October 30, 2015

Tanzania's new president, 'The Bulldozer' Magufuli


John Pombe Magufuli, pictured on October 21, 2015, is a former chemistry teacher

Dar es Salaam (AFP) - Tanzania's new leader John Pombe Magufuli rose from humble beginnings to win the presidency of east Africa's most populous nation in the country's hardest ever fought elections.

The win, on his birthday, by the 56-year old former chemistry teacher cements the long-running Chama Cha Mapinduzi (CCM) party's firm grip on power, ruling Tanzania since 1977 when two independence-era parties merged.
The elections, held on Sunday, were the hardest fought electoral race in the east African nation's history, with the opposition providing the first credible challenge to the CCM since the introduction of multi-party democracy in 1995.
But while the CCM will celebrate Magufuli's win, it came at the cost of several veteran CCM ministers and politicians, ousted from their parliamentary seats.
Magufuli won 58 percent of votes -- a total of 8.9 million -- compared to his closest rival Edward Lowassa, a former prime minister and CCM stalwart turned opposition chief who won 40 percent.
Magufuli's running mate Samia Suluhu Hassan, will become the first female vice president of Tanzania.
The opposition rejected the result, claiming victory itself, while the Zanzibar archipelago annulled polls over irregularities.
Minister of works in the last government -- for which he earned the nickname "The Bulldozer" -- Magufuli was not initially seen as a frontrunner, but won the CCM nomination from a field of nearly 40 other candidates.
He succeeds President Jakaya Kikwete, who stepped down from power having served his constitutional two-term limit.
- 'I know what it means to be poor' -
In a bid to show his strength and refute allegations he was not physically fit for the top job, during his campaign trail he performed push-ups to cheering crowds.
Running on an anti-corruption platform, Magufuli tried hard to cultivate an image of humility, and in rallies repeatedly asked supporters to let him work for them.
"Please allow me to be your servant, give me this great chance to serve you," he said, a message repeated in multiple campaign rallies.
He has also stressed the ordinariness of his upbringing.
"Our home was grass thatched and like many boys I was assigned to herd cattle, as well as selling milk and fish to support my family," he told one of his final campaign rallies.
"I know what it means to be poor. I will strive to help improve people's welfare."
Magufuli, who comes from Tanzania's northwestern Chato district, on the shores of Lake Victoria, was awarded a doctorate in chemistry from the University of Dar es Salaam. He spent some time studying at Britain's University of Salford.
A member of parliament since 1995 and a devout Roman Catholic, he has also taught in a secondary school and as an industrial chemist.
He has held various cabinet portfolios, including livestock, fisheries and land.
Many opposition supporters said they had had enough of CCM's decades-long dominance over Tanzanian politics, but supporters point out that the loser Lowassa did not represent much of a break with the past.
Lowassa, a long-time CCM loyalist before defecting, resigned as prime minster in 2008 over corruption allegations that he denied.
Magufuli's supporters say he offers hope for a different type of politician in Tanzania.
"He was for many years minister for works, supervising execution of mega projects worth trillions of shillings, but was never implicated in any corruption scandal," ex-prime minster and veteran CCM politician Joseph Warioba said of Magufuli.
"He could have been the richest politician in the country."

Source AFP

Thursday, October 29, 2015

NIMEKIPENDA KIMSHONO CHA GENEVIEVE NNAJI

kamshono kazuri eti eeh!

JK AMPONGEZA RAIS MTEULE DK. MAGUFULI IKULU, DAR JIONI HII


jk 2  
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza kwa furaha mshindi wa kinyang'anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakifurahia matokeo mara baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kutangaza kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii Oktoba 29, 2015.

jk

BREAKING NEWS: DK. MAGUFULI NDIYE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BREAKINGNEWS3
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Dk. John Pombe Magufuli kuwa ndiye Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 8,882,935  sawa na asilimia 58.46%.

Dk. John Pombe Magufuli.

Wednesday, October 28, 2015

DIAMOND: KAWEKA HISTORIA ULAYA



Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.

OKTOBA 25, mwaka huu ilikuwa ni moja kati ya siku za kihistoria nchini kwa Watanzania wote kujumuika na kupiga kura za kuwachagua wabunge, madiwani na rais.


Siku hiyohiyo pia katika Jiji la Milan, Italia kulikuwa na tukio la kihistoria kwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye alikuwa akiiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla katika Tuzo za MTV Europe Music (EMA) na kufanikiwa kuibuka na ushindi kupitia kipengele cha Best Worldwide Act: Africa/India ambacho alikuwa akichuana na mwanamuziki maarufu wa India, Priyanka Chopra aliyewahi kuwa pia Miss World mwaka 2000.
Uso kwa uso na mastaa ulaya
Kati ya matukio ambayo Diamond anasema hawezi kuyasahau ni pamoja na kupata shavu la kukutana na mastaa kibao wa ulaya ambao walipafomu na wengine kuchukuwa tuzo.
“Nimekutana na mastaa wengi ambao sikuwahi kukutana nao kabisa zaidi ya kuwaona tu kwenye mitandao na TV. Mastaa hao ni pamoja na Jason Deluro ambaye pia alipafomu Wimbo wa Want to Want, Pharrel Williams naye alipafomu Wimbo wa Freedom.“Nilipata bahati pia ya kuwashuhudia mastaa wengine kama vile Justin Bieber, Ed Sheeran na wengine kibao,” alisema Diamond.
Bieber anyakua 5 kwa mpigo
Staa wa Pop, Justin Bieber aliweka historia kwake katika tuzo hizo baada ya kuibuka na tuzo tano kwa mpigo.
Staa huyo aliyepanda jukwaani na kupiga ngoma yake mpya ya What Do You Mean alifanikiwa kuibuka na tuzo katika vipengele vya Best Male, Best Look, Worldwide Act: North America, Biggest Fans na Best Collaboration.
Mastaa wengine waliochukua tuzo hizo ni Nicki Minaj, One Direction, Macklemore, Taylor Swift, Ed Sheeran, Rihanna na wengine kibao.
Wazungu wapagawa na Diamond
Katika hali ya kushangaza mapema kabla ya kuanza kwa sherehe hizo za utoaji tuzo, Diamond aliyekuwa amevalia suti nyeupe alitinga ‘red carpet’ na kushangaa kuvamiwa na wazungu waliookuwa wamepanga foleni kuwasubiri mastaa huku kila mmoja akiwa na simu yake mkononi akitaka kupiga picha naye (selfie).
Washindi waliopita
Katika kipengele alichoshinda Diamond, alitanguliwa na Abdelfattah Grini (Morocco) aliyechukuwa mwaka 2011, Ahmed Soultan (Morocco) mwaka 2012 na 2013 na wa mwisho alikuwa Mohamed Assaf (Palestina).
Diamond anasemaje?
Kutokana na ushindi huo uliokuja Tanzania na Afrika kwa ujumla, Diamond alifunguka mengi ya kushukuru kwa wale wote waliompigia kura na kuahidi kufanya makubwa zaidi ya hayo katika kazi zake za muziki.
“Nimeshangazwa sana kwa namna ambayo nimepokelewa kwa kishindo nchini Italia. Wazungu wamenionesha thamani ya juu kwa mapokezi makubwa na kunishangilia na kunipongeza kwa tuzo niliyoipata. Nasema asanteni sana Watanzania wenzangu kwa sapoti mlionionesha mwanzo mwisho hadi kwa kunipigia kura na kufanikiwa kuibuka mshindi kutoka Afrika,” alisema Diamond.
Diamond alifanikiwa kupita tano bora Afrika katika Tuzo za Ema baada ya kupigiwa kura za kutosha na mashabiki wake kupitia mtandao wa Twitter. Wasanii wa Afrika aliokuwa akichuana nao kabla ya kutua Italia ni Yemi Alade (Nigeria), Davido (Nigeria), AKA (Afrika Kusini) pamoja na Wizkid (Nigeria).

Kutoka www.urambonews.com
Nakupongeza kwa ushindi wa tuzo hii Diamond. Hakika unaendelea kupeperusha vyema nchi yetu ya Tanzania. Mwenyezi Mungu azidi kuwafungulia milango na wasanii wengine wote ili nchi yetu izidi kung"ara zaidi.

BREAKING NEWS: ZEC YAFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR

uchaguziMwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi  Zanzibar, uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Jecha amesema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Uchaguzi huo utarudiwa baada ya siku 90.

TAARIFA ZAIDI HAPA CHINI




SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

Monday, October 19, 2015

Kweli mapenzi yana nguvu. neno i love you lamzindua lamzindua Lamar aliyekua amepoteza fahamu tangu oktoba, 13.




Lamar Odom.
 
MUNGU mkubwa! Lamar Odom mwishoni mwa wiki hii aliamka baada ya kupoteza fahamu kwa zaidi ya siku tatu, kwa madai ya kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya, lakini Ijumaa iliyopita alizinduka baada ya kusikia sauti ya mkewe, Khloe Kardashian, akimwambia ‘I love you’.
Lamar, 35, ambaye ni staa wa zamani wa NBA, aliripotiwa kupoteza fahamu tangu Oktoba 13, mwaka huu na kulazwa kwenye Hospitali ya Sunrise huko Las Vegas huku aliyekuwa mkewe, Khloe akionekana kuwa naye karibu sana.
Hata hivyo, Khloe ambaye alikuwa akifuatilia talaka mahakamani ili aachane na Lamar, ameonekana kusitisha ili aweze kuwa karibu zaidi na mumewe huyo wa ndoa kwa kipindi hiki kigumu.Lamar ana watoto wawili ambao alizaa na aliyekuwa mpenzi wake, Liza Morales, ambao ni Destiny, 17 na Lamar Odom Jr, 13.

Wednesday, October 14, 2015

SHERIA YA MTANDAO YAMGUSA MWINGINE MKOANI DODOMA



Mtayarishaji wa vipindi, Sospiter Jonas amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma Mjini akishtakiwa kwa matumizi mabaya ya mtandao.
Sospiter alisomewa mashtaka hayo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mussa mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Emmanuel Bwile.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook ujumbe kuwa “Pinda utakuwa muhubiri wa injili tu.”
Mussa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo alibandika picha ya John Maliga kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika ujumbe huo, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu namba 16 cha Sheria ya Mtandao ya Mwaka 2015.
Mlalamikaji katika shauri hilo la jinai namba 815/2015 litakalokuja tena mahakamani Oktoba 19, ni John Maliga.
Mshtakiwa yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya Sh1 milioni.
Kesi hii imekuja baada ya wiki iliyopita, kijana mmoja, Benedict Ngonyani (24) kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange.
Kijana huyo anatuhumiwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook na WhatsApp kuwa, Mwamunyange, amelazwa kwenye hospitali moja mjini Nairobi, Kenya kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu

Jamani, aliyetuumba hajatukosea. Why all this?

Nashauri wamama na wadada tuachane na mambo kama haya ya kutumia viungo bandia katika miili yetu. Ni vizuri tujipende na kujivunia vile ambavyo Mungu ametuumba kwani hajatukosea. Haya, umeweka maziwa kama haya ya bandia, halafu ukapata shemeji, mkifika chumbani inakuaje sasa? Maana pengine shemeji alivutiwa na hayo manyonyo bandia uliyojipachika halafu afike chumbani anakuta ni fake, sijui uso wako utauweka wapi. Aliyetuumba hajatukosea jamani eeee!

My dear fellow women, will you be able to try this Snail Beauty Treatments ? Me I can't ooh!

I copied it from somewhere....

I have been obsessed with beauty products from a young age.Really bad I know! But, for about two years now, I found a new obsession with natural skin care procedures.Last week, I decided to attend the Beauty Africa Exhibition Expo at Eko Hotel in Lagos.. I happened to walk  during the session of a gorgeous beautician (Gosh I hate that I've forgotten her name.)She said she was 50 and didn't look it one bit...No wrinkles, her hands ,soft and supple and she had the richest dark skin I had ever seen.

While I  listened to her natural beauty tips and took some notes,I heard her say "Snails"...The gasps from those in attendance said it all.
Yes..She said snail slime smooths out wrinkles,tightens the face and removes impurities..Infact she kept gushing about the wonders of snail treatment on the face..

That wasn't going to be a problem.All I needed to do was go buy some live snails,extract the slime and apply on my face for an hour,wash off and viola...My face instantly lifted..As she said with that,you have an instant face lift equal to botox..

I was just about to rush out when I heard her say,and remember, the most effective is when you let the live snail crawl on your face...
Ewwwwwwwww arrrrrhhhhhggg whooouuuuuuuuu the crowd echoed ..

The thought of those slimy creatures,crawling on my face all in the name of sucking out impurities was not imaginable..
On a second thought,beauty is pain right? I have seen ladies do worse for beauty, even having snake massages(yep! Leave that for another day)...It can't be worst than vampire facials,or botox injections..

I decided to do some research on it before trying it out .Many have attested to it's potency..I finally bought my snails last night..Looking at them carefully bringing one up to my face,with trembling hands I said a silent prayer..Hoping this is the beginning of a beauty romance between my face and slimy snail..

I closed my eyes and dropped the first one.I screamed silently and it stuck to my face..5 minutes later, I removed them,left the slimy residue for 2 more hours ..
When I washed my face with warm water and salt for disinfection,I smiled at the results..It did work.But was it worth it ? Well, let's just say,any day I'm up to it.

FLORA MBASHA AKIRI: MWANANGU SI WA MBASHA!




OHOOO! Kimenuka tena. Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amesema mwanaye mdogo (jina linahifadhiwa) hahusiani hata kidogo na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha huku akidai kuwa anamtambua mwanaume huyo kama mzazi mwenzake kwa mtoto mmoja tu (Liz), Risasi Jumatano linakupa zaidi.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha na aliyekuwa mumewe, Emmanuel Mbasha.

Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki, Flora alisema amechoshwa na manenomaneno yanayosemwa juu yake na Emmanuel na kwamba kama mumewe huyo ameamua kumwaga ugali, yeye yupo tayari kumwaga mboga.
Mwimbaji huyo alisema kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa anampenda mumewe na kwamba yupo tayari kuishi naye haikutoka moyoni, isipokuwa alifanya hivyo kwa huruma tu, kwa sababu mwanaume huyo ni mtu katili, mwenye roho mbaya na asiyemuogopa Mungu.
“Mtu mwenyewe alimtelekeza mtoto (Liz) kwa zaidi ya mwaka mmoja, ni mtu mbaya sana, sina mapenzi na Mbasha hata kidogo, ni afadhali niolewe na chizi anayeokota makopo kuliko kurudiana na mtu katili na mnyama kama huyo, namheshimu kama mzazi mwenzangu kwa Liz,” alisema.
Mtoto anayedaiwa kuibua mazito.

“Huyo mwanaume hafai kabisa, ni katili, namfananisha na shetani, anajifanya mwema kwa watu wakati hajawahi kuiomba msamaha familia, sikubaliani kabisa na hukumu ya mahakama, ukweli anaujua kwamba alibaka na hata mkimtaka huyo binti mumhoji nitamleta, isitoshe sasa hivi hata mtoto wake hamjali, hajui anasoma vipi, hajawahi kulipa hata shilingi ya ada, mimi mwenyewe ndo nahangaika kumlea mwanangu Liz ambaye anasoma kidato cha kwanza.
“Hastahili kabisa kuitwa baba sababu mzazi mwenye akili hawezi kutelekeza familia hata kama tumegombana, nimemwachia nyumba niliyojenga kwa pesa yangu na pesa zote aliweka kwenye akaunti yake na zote nilimwachia lakini kashindwa kuihudumia familia.”
Flora anajulikana kuwa na watoto wawili, mdogo akiwa ni yule aliyezaliwa wakati wanandoa hao wakiwa katika mzozo uliosababisha watengane hadi hivi sasa. Alipoulizwa kwa nini anadai aliyekuwa mumewe kumtelekeza mtoto mmoja tu, badala ya wawili, alifunguka.
“Huyu mwanangu mdogo hausiki naye kabisa, tena asiwe anamtaja kabisa kwa sababu hamhusu, hajui hata matumizi yake yakoje, mengine kaka achana nayo tu,” alisema Flora.
Mwimbaji huyo mwenye kipaji alipoulizwa sababu za kufuta kesi ya kudai talaka, aliyoifungua hivi karibuni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati anadai hamtaki na hawezi kurudiana naye, alisema alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na mtu ambaye hata hivyo, alikataa kumtaja.
Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha.

Flora alisema familia yake haijaridhishwa kabisa na suala la kesi ya ubakaji iliyokuwa ikimkabili mumewe kumalizika kwa kuachiwa huru na kwamba wanajipanga kwa ajili ya kukata rufaa.“Hiyo kesi imeisha kisiasa, Mbasha aliwahi kukiri kuwa ni kweli alifanya kitendo hicho, iweje leo aonekane hana hatia? Tutakwenda kukata rufaa ili haki itendeke.”
Baada ya kuzungumza na Flora, mwandishi wetu alimtafuta Mbasha kwa lengo la kumuuliza kuhusu madai ya mtoto yule mdogo kutohusika naye kama alivyosema mkewe, naye bila ‘kutafuna maneno’, alisema hata yeye hamtambui huyo mtoto mdogo, ila anaomba arudishiwe mtoto wake mkubwa, Liz na maisha mengine yaendelee.
“Hata mimi simtambui huyo mwingine, ninachoomba anirudishie tu mtoto wangu mkubwa Liz, huyo mwingine sihusiki naye kabisa kama alivyosema, yeye (Flora) ndiye anajua mhusika wa huyo mtoto, lakini si mimi na wala hajakosea kusema hivyo, nililitambua hilo tangu zamani, anipe tu mwanangu wa kwanza,” alisema Mbasha.
chanzo: global publishers

Tuesday, October 13, 2015

Maelezo ya Wizara kuhusu umiliki wa mitambo ya kuzalisha umeme

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi.

Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme yote nchini ni ya kampuni binafsi bali alichosema ni kuwa, baadhi ya mitambo ni ya kampuni binafsi na mingine inamilikiwa na Serikali.
Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:-

  1. Kinyerezi I (Gesi) yenye uwezo wa MW 150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12 Oktoba 2015;
  2. Ubungo I (Gesi) yenye uwezo wa MW 102 ambayo kwa sasa inazalisha MW 85;
  3. Ubungo II (Gesi) yenye uwezo wa MW 105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
  4. Tegeta (Gesi) yenye uwezo wa MW 42 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
  5. Nyakato (Mafuta) yenye uwezo wa MW 60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
  6. Kidatu (Maji) yenye uwezo wa MW 204 ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;
  7. Kihansi (Maji) yenye uwezo wa MW 180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;
  8. Pangani (Maji) yenye uwezo wa MW 68 ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;
  9. Nyumba ya Mungu (Maji) yenye uwezo wa MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha MW 5;
  10. Hale (Maji) yenye uwezi wa MW 21 ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na
  11. Mtera (Maji) yenye uwezo wa MW 80 ambapo mitambo yake imezimwa (MW-0);
Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870 zinazotakiwa kuzalishwa.

Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:-

  1. IPTL (Mafuta) yenye uwezo wa MW100 ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;
  2. Aggreko (Mafuta) yenye uwezo wa MW 70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
  3. SONGAS(Gesi) yenye uwezo wa MW180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 158; na
  4. Symbion (Gesi) yenye uwezo wa MW 112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.

Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha umeme wa kiasi cha Megawati 382 kati ya Megawati 462 zinazohitajika.

Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha mitambo hiyo yote inayomilikiwa na Serikali na Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao umepungua kutoka MW 561 hadi MW 88. Ili nchi isiwe na mgawo wa umeme zinahitajika MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme kinachopatikana ni Megawati 719.

Awali tulikuwa na upungufu wa megawati takribani 450 lakini tumefanya juhudi za kuwasha mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa upungufu uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.

Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia kipindi hiki cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali kuwasha mitambo iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20 Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa umeme itaanza kutengemaa.

Asanteni na poleni kwa usumbufu unaojitokeza.

Imetolewa na;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Wanafunzi wataka Nec kutafuta ufumbuzi wapige kura

 

Wanafunzi wa Shule ya Arusha Sekondari wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutafuta ufumbuzi kwa wanafunzi waliojiandikisha vituo tofauti na walipo sasa ili waruhusiwe kupiga kura.

Waliyasema hayo wakati wa mafunzo ya elimu ya uraia na mpigakura yaliyotolewa na Taasisi ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) jana.

Katika mchango wake kuhusu elimu hiyo, mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo, Glory Kamwela, aliiomba serikali kurekebisha kasoro za uandikishaji zinazosababisha wanafunzi wa shule za bweni na taasisi za elimu ya juu, kukosa haki ya kupiga kura kutokana na kujiandikisha maeneo tofauti na wanayokuwapo siku ya kupiga kura.

Alisema kwa mfano wanafunzi wengi mwaka huu watakosa haki ya kupiga kura kutokana na baadhi kujiandikisha maeneo tofauti na wanapokuwapo siku ya kupiga kura.

“Serikali lazima irekebishe hali hii kwa chaguzi zijazo,” alisema.

Kwa upande wake, Naylah Ally, anayesoma kidato cha sita, alivitaka vyama vya siasa, wagombea na taasisi zinazohusika na utoaji wa elimu ya uraia, upigaji kura na kunadi sera kuelekeza nguvu maeneo ya vijijini.

“Huko ndiko wanakoishi wapigakura na wananchi wengi wanaokabiliwa na changamoto ya mawasiliano na upatikanaji wa habari,alisema.

Alisema kampeni na harakati nyingi za kisiasa na uchaguzi hufanyika mijini ambako kuna mfumo rahisi wa mawasiliano huku maeneo ya vijijini yakisahaulika au kutopewa kipaumbele.

Wanafunzi hao walisema somo la uraia linalofundishwa sasa hivi shuleni lina upungufu wa mkazo wa eneo la muhimu la uzalendo, uadilifu na uwajibikaji katika jamii.

Maafisa kutoka taasisi hiyo, Zulekha Ibrahim na Dianarose Leonce, waliwataka wanafunzi na vijana wote wenye umri na sifa ya kupiga kura kuchanganua hoja, sera na ahadi za wagombea na vyama.


Rais wa Serikali ya wanafunzi shuleni hapo, Innocent Benjamin, alisema elimu ya uraia na uzalendo itawajengea vijana uwezo wa kujitambua mapema.