LATEST POSTS

Monday, July 22, 2013

MJUMBE WA BARAZA LA KATIKA ALALAMIKIA WANAWAKE WA TANZANIA BARA KUWACHUKULIA WAUME ZAO


Mjumbe wa Baraza la Katiba wa Wilaya ya Unguja Kaskazini Bibi Asha Haji Juma ametaka Katiba Mpya iwe na kifungu kinachopinga Wanawake kutoka Tanzania Bara kuwa na mahusiano au kuolewa na Wanaume kutoka Zanzibar.


 
 Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akizungumza wakati wa kujadili rasimu ya Katiba Mpya kwenye Mkutano uliofanyika katika kituo cha mafunzo ya ufundi stadi Mkokotoni, Bibi Asha Haji Juma alisema kwanini rasimu hiyo ya Katiba Mpya haina kifungu kinachozuia Wanawake kutoka Tanzania Bara kuwa na mahusiano ama kuolewa na Wanaume wa Zanzibar kwani kitendo cha wanawake wa Bara kuwa na mahusiano ama kuolewa na Wanaume wa kizanzibar, kinapelekea waume zao kupunguza mapenzi kwao.
"Sisi hatuna tena raha na waume zetu kwani wanawake wa Bara wanapokuja na kuwa na mahusiano na waume zetu, husababisha waume zetu kupunguza upendo kwetu na kututelekeza. Aliendelea kulalamika kuwa, miaka mitano iliyopita, kundi la wanawake kutoka Unguja Kaskazini walilalamika kwamba, wanawake kutoka Tanzania Bara wanawaibia waume zao. Inaaminika kuwa, wanaume wa kizanzibar hasa walio katika maeneo ya utalii ambao wana mahusiano na wanawake wa Tanzania Bara, wanakuwa wanaendeshwa na wanawake hao. Hii si haki".alilalamika Bi Asha.

Chanzo: Allafricanews.


0 comments: