MATESO kila
kukicha. Kijana Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma
mjini, Mkoa wa Mara yuko katika mateso makubwa baada ya tumbo lake
kuvimba na kuongezeka ukubwa hali inayomfanya ashindwe kutembea.
Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma mjini.
Shaggy Sadick mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Musoma mjini.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa, dada wa Shaggy, Mariam Sadick,
alisema mdogo wake alianza kuumwa ugonjwa huo tokea akiwa na umri wa
miaka 12 na kwa muda wote huo, wamehangaika katika hospitali mbalimbali
nchini bila mafanikio.
Alisema awali walianza kumpeleka katika Hospitali ya Musoma na baadaye Bugando jijini Mwanza ambako baada ya vipimo, iligundulika kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambao umejaa maji, ugonjwa ambao anapaswa kutibiwa nje ya nchi ili kuumaliza.
Alisema awali walianza kumpeleka katika Hospitali ya Musoma na baadaye Bugando jijini Mwanza ambako baada ya vipimo, iligundulika kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambao umejaa maji, ugonjwa ambao anapaswa kutibiwa nje ya nchi ili kuumaliza.
“Kwa kweli tumehangaika naye sana kumsaidia apone, lakini
imeshindikana kwani ili apone, wanapaswa kumpeleka nje ya nchi kwa
matibabu, kitu kinachotishia uhai wake kwani familia ni duni,” alisema
dada huyo.
Dada huyo alizidi kulia kwa kusema kwamba kingine kinachomsikitisha
ni kwamba mdogo wake amekosa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu
kwani kwa matatizo aliyonayo, hawezi kutembea tumbo limefika hadi
magotini.
Alisema wakati wa kulala ukifika, mdogo wake hupata wakati mgumu
kwani wanalazimika kumuwekea mito mingi ya kulalia nyuma yake,
vinginevyo anaweza kupoteza maisha kwa sababu ya kushindwa kupumua
vizuri.
“Kwa kweli kitu ambacho kinatusikitisha wote ni kukosa kufanya
mtihani wa kidato cha nne, maana hawezi kutembea tena wakati wa kulala
ndiyo kama hivyo,” alisema.
Mtoto Shaggy yupo katika mateso makali sana, anahitaji msaada wa
hali na mali ili aweze kuyaokoa maisha yake ili apate matibabu, endapo
utaguswa na habari yake, wasiliana na chumba cha habari kwa namba 0713
612 533.
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
0 comments:
Post a Comment