LATEST POSTS

Saturday, November 23, 2013

UJENZI WA BARABARA YA MOROGORO KUKAMILIKA 2014.

KUSEMA UKWELI, TUMETOKA MBALI. HAPA TULIPOFIKA, TUMEPIGA HATUA.

Moja ya kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi kilichopo Magomeni Usalama jijini Dar.

Barabara ya Morogoro ilivyo sasa.…

Moja ya kituo ambacho kitatumika kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi kilichopo Magomeni Usalama jijini Dar.

Barabara ya Morogoro ilivyo sasa.

Njia ambayo itatumika kwa ajili ya magari madogo huku pembeni kikionekana kituo kwa mbali.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi huo.

Meneja wa mradi huo Deo Muta akisikiliza maelezo kutoka kwa walinzi DART wanaolinda vituo hivyo wanaozuia watu wasifanye biashara na wala kupita ndani ya vituo.

Naye akitoa yake ya moyoni kuwa kuna walinzi hawafanyi kazi kama walivyopangiwa majukumu yao.

Eneo la Manzese likionekana kwa mbali.

 
Eneo hilo likionekana kwa ukaribu zaidi.

Daraja linalojengwa katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo.

                      Daraja hilo likionekana lilivyoingia hadi ndani ya kituo.
 
UJENZI unaoendelea katika Barabara ya Morogoro, jijini Dar utakamilika ifikapo mwakani.
Akizungumza na mtandao huu meneja wa mradi huo kutoka DART, Deo Muta ‘Mzee wa Mi’ alisema kuwa ifikapo katikati ya mwaka 2014 mradi huo wa kutengeneza barabara kwa ajili ya mabasi yaendayo kasi utakuwa umekamilika kutokana na jinsi ujenzi unavyokwenda haraka haraka.
“Sisi kama DART tunategemea kukabidhiwa barabara na Kampuni ya STRABAG inayojenga  katikati ya mwaka 2014 hivyo tunawaomba wanachi hasa wanaokaa au kufanya biashara pembezoni mwa barabara hii waendelee kuwa kando na watuvumilie  hadi pale mradi huu utakapokuja kukamilika hiyo mwakani” alisema Deo Muta.
RESOURCE: GLOBAL PUBLISHERS

0 comments: