CHAMA cha watumishi wa serikali Kuu na Afya,TUGHE,Mkoani
Tabora,kimeeleza kuwa hakitawatetea watumishi wanaokwenda kinyume cha
sheria,kanuni na taratibu za kazi zao.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Mkoa wa Tabora,Bw.Ezra Lema,amesema kutokana na hali hiyo
watumishi ni lazima wafuate mikataba yao ya ajira na kama inatokea wanaonewa
hapo chama chao kitawatetea kwa nguvu zote.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji Mkoa,Mwenyekiti huyo
amesema chama chake kitawatetea watumishi ambao waajiri wao hawakutimiza wajibu
wao baada ya wao kutimiza wajibu wao.
Akiwazungumza
viongozi wa matawi,Bw,Lema amesema ni muhimu wakapata elimu ya mahusiano kazini
ili wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi tofauti na ilivyo sasa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa wanawake wa chama hicho mkoa wa Tabora,BI. Plaxeda
Mkwira, amesema wanawake wa chama hicho wengi hawajui haki zao na wanafanya
jitihada za kuwaelimisha kuzijua haki zao.
Kikao hicho pia kiliazimia kwa viongozi kutembelea wanachama wao kwenye matawi
na kutoa elimu kwao kwani ndio muhimu na kukifanya chama hicho kuwa imara
zaidi.
SOURCE: TABORA YETU
0 comments:
Post a Comment