LATEST POSTS

Friday, April 17, 2015

Watu 10 wakamatwa msikitini wakiwa na milipuko, sare za jeshi, bendera ya Al Shabaab

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya milipuko 30 inayodaiwa kukamatwa baada ya polisi kuwakamata watu 10 katika eneo la Kidatu, mkoani humo. Picha na Lilian Lucas
Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea Aprili 14 mwaka huu majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani  Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua kufatilia nyendo zao.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu ambao walipata taarifa wapo katika Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu ambao wanatiliwa mashaka,”
Alisema polisi waliendelea na ukaguzi na kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo na kuwatia nguvuni.
Chanzo: Mwananchi

0 comments: