Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamepeleka mapendekezo ya kuigawa kuwa na halmashauri mbili.
Mapendekezo hayo yalifikiwa kwenye kikao cha baraza maalumu la madiwani kilichoketi makao makuu ya wilaya, Kata ya Isikizya.
Katika kikao hicho madiwani wote walichangia michango yao ambapo walishauri kwa kauli moja kuwa wilaya hiyo igawanywe na kuwa na halmashauri mbili za Tabora na Igalula.
Wakichangia kwenye mjadala huo walisema kugawanywa wilaya hiyo kuwa na halmashauri mbili ni faida kwa wananchi, hasa ikizingatiwa hali ya jiografia kwenye wilaya hiyo siyo nzuri.
“Agizo letu kama madiwani tunapeleka mapendekezo ya kuwa na halmashauri mbili za Igalula na Tabora. Hii itasaidia kusogeza huduma kwa wananchi wetu,” alisema mmoja wa madiwani hao.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment