LATEST POSTS

Sunday, January 12, 2014

Majina matatu ya Wanawake watatu Tanzania ambao wanaweza kugombea Urais haya hapa

Mhe. Anna Abdallah, amewataja  Mhe. Asha Rose Migiro, Mhe. Anna Makinda na Mhe.Anna Tibajuka kuwa ndio wanawake ambao wanaweza kusimama kugombea kiti cha Urais Tanzania. " Wapo wengi lakini hawa ndio ambao nimeweza kuwataja kwa sasa". Alisema Mhe. Anna Abdalla alipokuwa katika mahojiano na mwandishi katika kipindi cha mwanasiasa wetu kinachorushwa na Star Tv kila siku ya Jumapili.

Sambamba na hilo, Mhe.Anna Abdallah aliwataka wanawake wajitokeze kugombea nafasi hiyo ya Uraisi kwani ni jambo ambalo linawezekana na hakuna mwanaume aliyeumbwa kwa ajili ya kuwa Raisi.

Haya sasa, kina mama mlio na sifa msisite kujitokeza katika mapambano haya ya kukalia kiti cha Uraisi.
               
                                   Spika Anna Makinda
                                                            Mhe. Anna Tibaijuka

0 comments: