Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Mahongoro Mahanga
akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashtaka
yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary) Bi, Itika Kasambala
katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi bila mkataba na
kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili tu.…
Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Mahongoro Mahanga
akitoka katika chumba cha mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi wiki iliyopita siku ya Jumanne baada ya kusomewa mashtaka
yake ya kumfanyisha kazi PS wake (Private Secretary) Bi, Itika Kasambala
katika ofisi yake ya Bunge kwa muda wa miaka kumi bila mkataba na
kusitisha kazi yake na kisha kulipa mafao ya laki mbili tu.
Naibu
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana akishuka katika kazi za
mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi wiki iliyopita siku
ya Jumanne jijini Dar es Salaam.
Bi. Itika Kasambala akiwa katika moja ya vyumba vya habari baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
Baadhi ya nakala za malada ya kesi hiyo iliyofunguliwa mahakama ya kazi, Tume ya Usuluhishi na Upatanishi na Bi. Itika Kasambala dhidi ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.
.Msaidizi wake wa ofisi ya Bunge afanya kazi miaka kumi chini yake bila mkataba
.Baada ya miaka kumi amlipa mafao ya laki mbili tu.
.Dada alalama kwamba Naibu Waziri alimtaka kimapenzi akakataa
.Baada ya miaka kumi amlipa mafao ya laki mbili tu.
.Dada alalama kwamba Naibu Waziri alimtaka kimapenzi akakataa
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dkt Makongoro Mahanga ameingia kwenye kashfa nzito ya kuvunja sheria za kazi nchini kwa kumfanyisha kazi msaidizi wake (PS) wa ofisi yake Bunge kwa miaka kumi bila mkataba na kumlipa fedha taslimu shilingi laki mbili tu (200,000) kama mafao.
Naibu Waziri, Mahanga anakuwa kiongozi wa
kwanza kuingia kwenye kashfa akiwa madarakani tena kwenye swala la ajira
wakati yeye mwenyewe ni waziri mwenye dhamana na masUala ya ajira na
haki za wafanyakazi nchini chanzo chetu kimeelezwa.
Kwa mujibu wa sheria kazi na mahusiano
kazini, Naibu Waziri amekiuka kifungu cha 3 cha sheria ya Taasisi za
kazi za mwaka 2004 na pia amekiuka sehemu ya tatu ya viwango vya ajira
na sehemu ndogo A kwa kushidwa kuandika mkataba kwa mujibu wa kifungu
cha 14 ibara ya kwanza kama sheria ya kazi na mahusiano kazini
inavyotaka.
Katika kifungu hicho cha 14 ibara ya kwanza
kinasema mkataba utakuwa wa kipindi cha muda usiotajwa, mkataba wa kazi
maalumu na mkataba unatakiwa kuwa wa maandishi ambapo vyote Mhe Naibu
Waziri hakufanya.
Ibara ya 15 kifungu cha.-(1) kinasema kwa
kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (2) cha kifungu cha 19,
mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, wakati mfanyakazi anapoanza kazi,
taarifa zifuatazo kwa maandishi, jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia
ya mfanyakazi; mahali alipoajiriwa; kazi zake; tarehe ya kuanza; muundo
na muda wa mkataba; kituo cha kazi; masaa ya kazi; ujira na njia ya
ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bi. Itika Kasambala (31) anasema
alianza kazi kwa Mbunge huyo wa Segerea na Naibu Waziri wa kazi Dkt.
Mahanga, mwaka 2003 kama PS (Personal Secretary) kwa makubaliano ya
kumpa mshahara wa shilingi 120,000 kwa mwezi lakini alianza kumlipa
shilingi 50,000 tu.
“aliniambia kwamba nianze kazi kwanza baadaye atanipa mkataba wa ajira na kunilipa mafao ya hifadhi ya jamii na matibabu lakini baada ya miaka kumi ananitumia sms akiwa Dodoma kwamba kazi basi sikuhitaji tena,” Kasambala alisema.
Amesema kwamba Mbunge huyo alimtumia sms
akiwa kwenye vikao vya bunge mjini dodoma mwaka jana mwezi wa sita
akimjulisha kwamba ajira yake imeshafika kikomo kwa sababu hana uwezo
tena wa kumlipa mshahara na mahitaji mengine ya kiofisi.
Kasambala aliendelea kusema kwamba mara ya
kwanza wakati anaanza kazi mwezi wa tano mwaka 2003 baada ya msaidizi wa
ofisi ya mbunge Mahanga kuacha kazi na ndipo alipotafutwa yeye na
walikwenda kuelewana kwa malipo ya 120,000 kwa mwezi.
Alisisitiza kwamba mara baada ya kuanza
kazi kwa ofisi ya mbunge alikuwa analipa pesa kupitia mkononi na baadaye
tigo pesa na baada ya muda akawa anachukua pesa yake ya mshahara toka
katika manisapaa ya Ilala kama posho ya Mhe Mahanga kama diwani kila
mwezi.
Dada huyo kwa mshangao baada ya mahojiano ya muda mrefu alikiri kwamba Mhe Mahanga alikuwa na nia ya dhati kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na kumtaka aende Dodoma lakini alikataa kufanya masharti hayo.
“mwaka juzi baada ya kuonyesha nia ya
kunitaka kimapenzi alinipigia simu akitaka niende Dodoma bungeni kwa
mazungumzo zaidi kama msaidizi wake lakini nilikataa,’ aliongeza
Kasambala.
Amesema tangu aanze kazi kwa Mhe Mahanga hakuwa anatoa huduma zozote kama matibabu au fedha kwa ajili ya sikukuu ilikuwa ni mshahara tu wa 120,000 kwa mwezi lakini kila akimfuata ili waandikishiane mkataba alikuwa akizungumsha bila sababu za msingi.
Bi. Kasambala aliongeza kuwa amefanya kazi
Mhe Mahanga tangu akiwa mbunge wa Ukonga na baadaye Segerea lakini
ameshidwa kuheshimu sheria za ajira na taratibu za kazi wakati yeye
mwenyewe ni waziri mwenye dhamana ya ajira kwa watanzania.
Amesema mwaka jana tarehe 14/09/2013
alimtumia kwa Tigopesa kiasi cha shilingi za Tanzania 200,000 kama mafao
yake baada ya kufanya kazi kwa takribani miaka 10 kama Msaidizi wake wa
Ofisi ya Mbunge.
Amesema kwamba aliamua kwenda Chama cha
Wafanyakazi wa Hifadhi, Mahoteli, Majumbani na Kazi Nyingine (CHODAWU)
kwa msaada wa kisheria na baada ya kukutanishwa bado Mhe Mahanga akawa
mgumu kukubaliana kiungwana mpaka ikawalazimu kwenda mahakamani Tume ya
Usuluhishi na Upatanishi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
wakili wa Kasambala, Nyaisa Godwin alisema kuwa kesi imefunguliwa
mahakama ya kazi wiki iliyopita siku ya Jumanne, Tume ya Usuluhishi na
Upatanishi kesi namba CMA/DSM/ILA/R.711/13.
Wakili Nyaisa alisisitiza kwamba Naibu
Waziri aliiambia mahakama kwamba Dada Kasambala alikuja kufanya kazi
kwake kama mwanafunzi wa chuo kwenye mazoezi lakini alishidwa
kuithibitishia mahakama kwa ushawishi wa barua ya (field toka chuoni).
“tulishagazwa na majibu ya waziri kwamba dada huyo alikuwa field, na nilimuuliza field ya miaka kumi? Alishidwa kutoa jibu mbele ya mpatanishi (Arbitrator),” amesema Nyaisa.
Chanzo: GPL
0 comments:
Post a Comment