Polisi mkoani Iringa, wanawashikilia watu sita kwa tuhuma tofauti.
Watuhumiwa hao ni pamoja na mwanamke mmoja wa
Iramba wilayani Mufindi, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kumchinja mtoto
wake na kumtupa chooni.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi, alisema mwanamke huyo amemchinja mtoto huyo kwa kutumia kitu chenye ncha.
Alisema sababu za mwanamke huyo kufanya ukatili
huo hazijajulikana na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini
chanzo chake.
Katika tukio lingine, watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na pembe tano za ndovu tano zenye uzito wa kilo 37.
Kamanda Mungi alisema “Hata hivyo thamani wa nyara hizo haijajulikana lakini watuhumiwa walikuwa wanatumia gari aina ya Premio.”
Watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo ya Ikweha
wilayani Mufindi.Alisema watuhumiwa ambao majina yao yamehifadhiwa kwa
sasa ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kwamba wanatarajia kufikishwa
mahakamani baada upelelezi kukamilika.
Wakati huohuo, watu wawili wakazi wa Mshine Tatu, mjini hapa wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na kete 16 za dawa za kulevya.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment