Dar es Salaam.
Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, wanawashikilia watu
watatu kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi Mwenyekiti wa Chadema wilayani
Temeke, Joseph Yona, ambaye baadaye, alitelekezwa Ununio, Kunduchi.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea mapema wiki hii.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Suleiman Kova, alisema kwa sasa watu hao wanahojiwa kabla ya
kuwafikisha mahakamani.
Alisema watuhumiwa, walikamatwa kwa nyakati
tofauti juzi na jana. “Tunawahoji na uchunguzi ukikamilika tutawafikisha
mahakamani,” alisema Kova.
Kamanda huyo alisema polisi pia wanaendelea kuwatafuta wahusika wengine wa tukio hilo.
Baada ya kujeruhiwa, Yona alifikishwa katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako katika simulizi zake alisema
alitekwa akiwa Mtoni kwa Aziz Ali.
Alisema alitekwa saa 5:00 za usiku na kuingizwa
katika gari moja kwa maelezo kuwa alikuwa anapelekwa polisi lakini
njiani alipigwa na kwenda kutelekezwa Ununio.
Alisema kabla ya kutekwa, alikuwa ameketi na
vijana wanne wa Tawi la Chadema la Ukombozi na kwamba ghafla
walijitokeza watu kama sita ambao walimnyanyua kwa madai kuwa alikuwa
anatakiwa polisi.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment