Mamlaka nchini Venezuela zimetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa pili wa juu wa chama cha upinzani nchini humo
Mratibu wa siasa wa chama cha Voluntad Popular nchini Venezuela, Carlos Vecchio
Jaji wa mahakama kuu mjini Caracas ameagiza kukamatwa kwa mratibu wa siasa wa chama cha Voluntad Popular, Carlos Vecchio akituhumiwa kuendelea kuhamasisha maandamano zaidi nchini humo kupinga Serikali.
Tangazo hilo la Serikali limeamsha maandamano zaidi nchini humo ambapo jana polisi walikabiliana na maelfu ya vijana kwenye miji mbalimbali nchini humo wakipinga kuendelea kushikiliwa kwa viongozi wao na kushinikiza rais Nicola Maduro ajiuzulu.
Siku ya Jumatano upinzani ulikataa kuketi meza moja na rais Maduro kwa kile walichodai wao sio watumwa wa Serikali yake bali wanawatumikia wananchi na watafanya hivyo pale tu atakapoondoka madarani.
Siku ya Jumatano upinzani ulikataa kuketi meza moja na rais Maduro kwa kile walichodai wao sio watumwa wa Serikali yake bali wanawatumikia wananchi na watafanya hivyo pale tu atakapoondoka madarani.
0 comments:
Post a Comment