Wabunge nchini marekani wameidhinisha mpango wa kuleta umeme
kwa zaidi ya watu millioni hamsini katika jangwa la Sahara barani Afrika na
hivyo basi kutoa fursa kwa mradi huo wa serikali ya Obama kuanza
kutekelezwa.
Mswada huo uliopitishwa na kamati ya maswala ya kigeni nchini humo unalenga
kujenga megawati elfu ishirini barani Afrika ifikiapo mwaka 2020 na kuwafikia
watu elfu hamsini ambao wanaishi bila umeme.
Mpango huo ulitangazwa na rais Obama wakati wa ziara yake barani afrika mnamo
mwezi juni mwaka jana.
Mswada huo utahitajika kupitishwa na bunge la wawakilishi pamoja na lile la
sineti lakini hatua hiyo ya kamati ya maswala ya kigeni ni dhihirisho tosha
kwamba unuangwa mkono na pande zote za kisiasa.
Chanzo: BBC Swahil
0 comments:
Post a Comment