Iwapo utamtikisa au kumgusa hali hiyo hupotea kwa sekunde kadhaa na kama atapata tena usingizi mlio huo hujirudia tena.
Si jambo geni kusikia mtu wako wa karibu au mwenza wako
anapokuwa amelala kuwa na kawaida akikoroma au kuwa na mikwamo mikwamo
ya milio isiyo ya kawaida akiwa katika usingizi mzito.
Iwapo utamtikisa au kumgusa hali hiyo hupotea kwa sekunde kadhaa na kama atapata tena usingizi mlio huo hujirudia tena.
Wengi wamekuwa wakijiuliza ni kipi husababisha
hali ya kukoroma na wengine wamelichukulia kuwa ni suala la kimaumbile
kama vile unene lakini sababu hasa wamekuwa hawaijui lakini kwa upande
wa afya linaweza kuwa ni kiashiria cha tatizo la kiafya mwilini.
Tayari kuna tafiti za sayansi ya tiba zinaonyesha
mahusiano makubwa ya magonjwa ya moyo na watu wanaokoroma au pingamizi
la usingizi.
Watu wenye pingamizi la usingizi hasa watu wazima wameonyesha kuwa na dalili za magonjwa ya moyo.
Pingamizi la usingizi ni nini?
Pingamizi la upumuaji usingizini ni hali ya kushindwa kupumua kwa kutumia pua au mdomo kwa muda wa sekunde kumi.
Tatizo hili hutokea zaidi ya mara 30 katika hatua
za vipindi viwili ambavyo kitaalamu hujulikana kama mjongeo wa kasi wa
macho na mjongea wa kawaida wa macho.
Mjongeo wa kasi wa macho wakati wa usingizi ni
kipindi kimojawapo cha usingizi wa kawaida ambacho huambatana na macho
kucheza cheza yaani mtu anakuwa yupo usingizini huku macho yake
yakicheza cheza.
Kwa kawaida wakati mtu amelala hupitia hatua hii mojawapo ya usingizi na hutokea mara nne hadi tano katika usingizi.
Hali hii huweza kutokea kwa muda mfupi na
mwishowe kipindi hiki hukawia kwa muda mrefu hasa inapokaribia asubuhi.
Inakisiwa kuwa mjongeo wa kasi wa macho huchukua asilimia 20-25 ya
usingizi wa mtu mzima yaani dakika 90-120 kwa ujumla.
Katika hali ya mjongeo wa kawaida wa macho ni
hatua ambayo mtu anakuwa amelala lakini hawezi kuchezesha macho, kuota
ndoto ni nadra sana kwa wenye kupata hatua hii. Akili huwa katika hali
njema kabisa viungo vya mwili wake kutolegea ndio maana mtu anaweza
kutembea huku akiwa usingizini. (sleep walk).
Tatizo la pingamizi la upumuaji usingizini huathiri zaidi wanaume kuliko wanawake.
Watu gani wako kwenye hatari ya tatizo hili?
• Unene uliopitiliza
• Shinikizo la damu (Hypertension)
• Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (Congestive Cardiac Failure)
• Matatizo katika mishipa ya damu ya moyo (Coronary Heart Disease)
• Unyongovu/sonona. (Depression)
• Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji (Chronic Obstructive Pulmonary Disease)
• Unywaji pombe kupita kiasi
• Uvutaji sigara kupita kiasi na matumizi ya madawa ya kulevya (ilicit narcotics)
• Historia ya mwana familia kuwa na tatizo hili.
• Watumiaji wa dawa zifuatazo: Barbiturates,
Benzodiazepines, Ethanol,hypertensive and diabetic treatment----kwa
kifupi dawa za usingizi, shinikizo la damu na kisukari.
Dalili na Viashiria
Vipimo Vya Uchunguzi
•Maumbile- wanaume wana viambo vidogo vya kupitisha hewa kuliko wanawake.
•Aina ya ulalaji, mtu anapolala chali, huzifanya nyama za koo kutulia na hivyo kuziba mianya ya upumuaji.
Dalili na Viashiria
• Kula zaidi kipindi cha mchana
• Kukoroma
• Ushuhuda wa mwenzi wako – wakati wa pingamizi la upumuaji au mitweto
• Kukosa usingizi kipindi cha usiku
• Uchovu
• Kuamka usiku kwenda kukojoa mara kwa mara
Vipimo Vya Uchunguzi
• Polysomnogram-kipimo cha picha kina choonyesha hali ya tishu za njiani ya hewa (puani).
• Actigraphy
Matibabu:
1. Muendelezo chanya wa shinikizo katika mfumo wa hewa
2. Matibabu ya matatizo yanayoweza kupelekea
kupata tatizo hili mfano kupunguza uzito kwa wale wenye uzito
uliopitiliza, kutibu shinikizo la damu, kupunguza unywaji wa pombe na
uvutaji sigara.
Lakini zipo dawa ambazo zimezagaa mtaani zinazodaiwa kuponya ukoromaji hata hivyo hazijathibitishwa kumaliza tatizo hilo.
Jambo la muhimu ni kufuata hatua muhimu na kujua chanzo kinachokufanya ukorome hasa kwa kuwashirikisha unaolala nao.
Kwa mfano waweza kumwambia unayelala naye
akuangalie wakati unaokoroma ni wakati gani na hivyo kujua chanzo. Hapo
utajua kipi kinasababisha ukoromaji wako na namna ya kukomesha.
Lakini kwa ujumla waweza kubadili aina ya kulala,
kwa mfano kuacha kulala chali, penga kamasi kabla ya kulala, safisha
chumba kabla ya kulala ili kuondoa hewa chafu inayoweza kusababisha
vumbi na hatimaye mikoromo.
0 comments:
Post a Comment