LATEST POSTS

Thursday, February 20, 2014

'Vimini' marufuku nchini Uganda

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha za watu wakiwa uchi.
Wanawake pia wamepigwa marufuku kuvaa sketi fupi au blauzi ambazo zinaonesha vifua vyao hadharani na kusababisha hisia za kingono.
Kwa mujibu wa BBC, Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kampala, Waziri wa Maadili na Utawala Bora, Reverend Simon Lokodo, alisema Rais Museveni alipitisha sheria hiyo Februari 6, miezi mwili baada ya Bunge kuipitisha.

0 comments: