Mmoja kati ya wataalamu kutoka nchini Vietnam wakiendelea na uchunguzi kuhusu kupotea kwa ndege ya Malaysia Airlines.
Wataalamu wanaoendesha uchunguzi kuhusu ndege ya Malaysia Airlines iliopotea siku sita zilizopita baada ya kupoteza mawasiliana wanasema hakuna dalili zozote za kutokea mlipuko ikiwa angani wakati huu Satalite za China zikigundua vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni kutoka katika ndege hiyo.
wataalamu wa China wamesema moja kati ya satalite kumi walizotuma kutafuta mabaki ya ndege hiyo wamegunduwa vifaa ambavyo vinasadikiwa kuwa ni vya watu waliokuwemo katika ndege hiyo iliotoweka tangu siku ya Jumamosi.
Operesheni hiyo ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo zimepanuliwa zaidi katika bahari ya Andaman katika eneo la magharibi mwa Malaysia mbali kidogo na eneo ambalo ndege hiyo inashukiwa huenda ndiko iliko angukia ikiwa na abiria 239.
Tayari Malaysia imetuma ndege zake katika eneo la anga ambalo satalite za China zimegunduwa mabaki ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya watu waliokuwemo katika ndege hiyo.
Wakati huo huo wataalamu wa Marekani wamesema hakuna viashiria vyovyote vinavyoonyesha kuwa kulitokea mlipuko katika ndege hiyo wakati ikiwa angani kabla ya kuanguka.
Ndege hiyo ya Malaysia iliokuwa ikisafiri kutoka jijini Kualalumpur kuelekea jijini Pekin nchini China ilipotea kimiujiza ikiwa angani na watu 239, huku wengi wao wakiwa ni raia wa China.
Zaidi ya nchi tisa zinashiriki katika opereshani ya kutafuta mabaki ya ndege hiyo ambapo hadi sasa juhudu hizo hazijazaa matunda.
0 comments:
Post a Comment