LATEST POSTS

Saturday, April 5, 2014

KADA CCM KATA YA USINGE AFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU SHITAKA LA KUISHI NCHINI AKIWA RAIA WA BURUNDI.

KATIBU wa Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Usinge wilaya ya Kaliua
mkoani Tabora Hassan Salumu Ntama ana kesi kujibu katika mahakama ya
hakimu mkazi mkoa wa Tabora baada ya kubainika ni mhamiaji haramu
mwenye asili ya nchi ya Burundi.
 
Katika cheti chake cha kuzaliwa kilikutwa na jina la Hassan Salumu
Ntala,wakati jina lake halisi ni Fredrick Ntala.
 
Kada huyo wa CCM amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kwa kesi
ya jinai namba 221/2014.
 
Katibu huyo wa CCM kata ya Usinge amefikishwa katika mahakama ya
hakimu mkazi wa Tabora Bahati Chitepo kwa makosa ya kuishi nchini
kinyume cha sheria namba S  kifungu kidogo cha sheria 31 (i) (i)  (2)
kifungu cha sheria za Uhamiaji kifungu cha 54 ya mwaka 2002.
 
Aidha kosa jingine ni kutoa taarifa za uwongo kwa afisa uhamiaji
kifungu kidogo cha  C/S  31 (i) (a) , (2) na kutumia cheti cha bandia
cha kuzaliwa kinyume cha kifungu cha sheria namba C/S 31(i) (e) 2.
 
Aidha Hassan Salumu Ntama alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza
mnamo mwezi machi 4 mwaka, 2014 ambapo upande wa mashitaka
uliwasilisha ushahidi wake kwa kuita mashahidi wawili.
 
Mashahidi wawili wa upande wa mashitaka walitoa ushahidi wao ni
Konstebo wa uhamiaji Marinta Morumba wilaya ya Urambo na katibu tawala
wa wilaya ya Urambo Pachael Byemela ili kuthibitisha makosa husika.
 
Hata hivyo kutokana na ushahidi wao mahakama imejiridhisha kutokana na
ushahidi wa upande wa mashitaka na kwa kuthibitisha kuwa katibu wa CCM
kata ya Usinge wilaya ya Kaliua Hassan Salumu Ntama ni mhamiaji haramu
toka nchini Burundi.
 
Aidha chini ya mwanasheria wa Uhamiaji mkoa wa Tabora Charles
Kasambula kada huyo wa CCM amepatina na hatia na anakabiliwa na kosa
la jinai itaanza kwa mshitakiwa kuanza kujitete mwezi April 6 2014.
 
Mapema mwaka mwaka jana mwishoni kufuatia zoezi la Operesheni Kimbunga
likiendelea kuripotiwa kuwa karibu uongozi wote wa kata ya Kaliua wa
chama cha mapinduzi ni wahamiaji haramu.
 
Taarifa hizo zilikuja kufuatia mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa
kufanya mkutano wa hadhara kata ya Usinge wilaya ya Kaliua na kuomba
wananchi kufichua wahamiaji haramu,majambazi na majangiri wanaoendesha
vitendo viovu.
 
Hatua hiyo inaonyesha kuzaa matunda baada ya kile alichotaka mkuu wa
mkoa wa Tabora kutaka wahusiska kufichuliwa hadharani ili sheria
ichukue mkondo wake.

0 comments: