LATEST POSTS

Tuesday, April 8, 2014

MASHINDANO YA SANAA, KUCHORA KWA WATOTO NA VIJANA KATI YA UMRI WA MIAKA 7 HADI 15

Haya watoto wetu, wenye vipaji vyenu jimwageni uwanjani. Hiyo milioni moja ikipatikana, mtapunguza ada shuleni. Kamateni fursa mwende zenu.


 
Amsha ubunifu wako!
Benki ya Dunia inawakaribisha watoto wa shule wa Kitanzania ambao ni wabunifu wenye umri kati ya miaka 7 hadi 15 kushiriki katika mashindano ya sanaa / kuchora, ambapo mchoro utakaoshinda utatumika kupamba jalada la mbele la Ripoti muhimu ya Benki ya Dunia kuhusu Tanzania.
Kaulimbiu ya shindano hili ni ‘Kazi kwa Watanzania Wote.’
Ni nani anaweza kuingia shindano hili?
Shindano liko wazi kwa watoto wote wa shule wa Kitanzania, wabunifu walio kati ya miaka 7 hadi 15.

Ninaingiaje kwenye shindano hili?
Unatakiwa kutumia mikono yako tu basi! Unaweza kuchora, kupaka rangi na michoro ya haraka haraka. Unaweza  kutumia peni, penseli, penseli ya rangi, mkaa, rangi ya mafuta, rangi za kikemikali (akriliki) au rangi za maji kutengeneza mchoro wako. Jaribu kuwa mbunifu, na tumia mawazo yako na fikra ili upate mchoro utakaofafanua kaulimbiu hii, ‘Kazi kwa Watanzania Wote.’

Je, naweza kushirikiana na mtu mwingine?
Ndio, unaweza kushiriki aidha kama mtu binafsi au kama timu (iliyo na watu wasiozidi 3).
Kipindi cha Shindano
Shindano linaanza tarehe 17 Machi 2014 na kuishia tarehe 17 Aprili 2014.

Je, kuna zawadi zozote za kushindaniwa?
Ndiyo! Mshindi atajinyakulia Shilingi Milioni Moja (1,000,000) na fursa kwa picha yake na maelezo ya maisha yake kutumika kupamba jalada la ndani la ripoti. Mshindi wa Pili atapata Shilingi 650,000; wakati Mshindi wa Tatu atapata Shilingi 350,000. Kila mshindi atapata shahada ya kutambuliwa kutoka Benki ya Dunia.

Nina maswali zaidi …
Endelea na yatume kwa barua pepe: unleash@worldbank.org na yatajibiwa ndani ya masaa 24 kama yatatumwa siku za kazi.

Sheria na Miongozo

1. Rika: Watoto wa shule kati ya umri wa miaka 7 hadi 15.

2. Ukubwa wa mchoro: Mchoro lazima ufanyike kwenye karatasi ya ukubwa wa A4 au A3.

3. Majina na Mawasiliano: Jina kamili, umri (siku, mwezi, na mwaka wa kuzaliwa), jinsi, na anuani kamili ikijumuisha namba ya simu na barua pepe (kama ipo) lazima iandikwe nyuma ya mchoro, na SIO juu ya mchoro.
4. Aina ya uchoraji: Unaweza kutumia mikono yako tu. Unaweza kuchora, kupaka rangi na michoro ya haraka haraka; tumia peni, penseli, penseli ya rangi, mkaa, rangi ya mafuta, rangi za kikemikali (akriliki) au rangi za maji.

5. Masharti ya kukubalika:
a) Kazi ambazo zimeonyeshwa au kukubaliwa sehemu nyingine hazitakubalika katika shindano hili.
b) Kazi ambazo zinaonyesha mtu maalumu, shirika au jina la biashara hazitakubaliwa.
c) Michoro iwasilishwe kupitia posta au kutumwa kupitia kampuni za kusafirisha vifurushi kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 17 Aprili 2014.
d) Michoro inatakiwa ipokelewe siku ya tarehe 17 Aprili 2014 au kabla.
e) Mchoro usiwe na maandishi au maelezo yoyote.

6. Aina ya mchoro unaokubalika: Nakala za michoro zilizoko kwenye karatasi au zilizotumwa kwa mtandao tu ndizo zitakazokubaliwa, ambazo hazina maneno wala maelezo. (*Angalia hapo chini)

7. Idadi ya michoro inayokubalika: Washiriki wanaweza kuwasilisha mchoro mmoja tu.

8.Watoto na ndugu wa wafanyakazi wa Benki ya Dunia hawaruhusiwi kushiriki katika shindano hili.

TAFADHALI ZINGATIA YAFUATAYO:
  HATIMILIKI  
Michoro lazima iwe ya asili na isiyonukuliwa kutoka sehemu nyingine kwa njia yoyote ile. Benki ya Dunia itakuwa na mamlaka juu ya hatimiliki zote za michoro iliyoshinda. Tuhuma za kuiba au kunukuu mchoro zitakuwa ni jukumu la mshindani pekee.

KUTANGAZWA KWA WASHINDI
Washindi wa shindano watatangazwa ndani ya wiki mbili baada ya tarahe ya mwisho ya kuwasilisha mchoro.

UWASILISHAJI
Tafadhali lete au tuma barua pepe ya wasilisho lako kabla au ifikapo tarehe 17 Aprili 2014 kwa anuani ifuatayo:

SHINDANO LA SANAA / KUCHORA Benki ya Dunia Mtaa wa Mirambo Na. 50 Dar es Salaam Tanzania Barua pepe: unleash@worldbank.org

0 comments: