Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Watanzania
wa Wisconsin wanapenda kutoa shukrani kwa wote waliojaribu kuokoa
kutokuchomwa moto kwa ndugu yetu, mpendwa wetu Mike Lukindo na pamoja na
jitihada zote zilizofanyika tunasikitika kuwataarifu kwamba, mpendwa
wetu ilibidi achomwe moto na jana Ijumaa April 4, 2014 majivu yake
walikabidhiwa familia yake kwa mtoto wa kwanza wa marehemu kwenda
kuchukua majivu hayo.
Mpaka
mazishi yafanyike zilikua zinahitajika $6,000 pamoja na michango ya sisi
tuliopo Madison, Wisconsin haikuweza kufikia idadi iliyokua
inahitajika.
Watanzania
wa Wisconsin wanavishukuru vyombo vya habari ndani na nje ya Marekani
vilivyosaidia kusambaza habari ya ndugu yetu, mpendwa mwenzetu na
Mtanzania mwenzetu mpaka habari kuwafikia ndugu zake Tanzania.
Shukrani
za pekee ziende kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani hususani Mhe. Balozi
Liberata Mulamula kwa mchango waliotoa na mara kwa mara Balozi kupiga
simu kufuatilia maendeleo ya msiba.
Sisi Watanzania wa Wisconsin kwa niaba ya familia tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawazidishia, Asanteni.
0 comments:
Post a Comment