MTANZANIA lilifanya jitihada za kumtafuta Siwa bila mafanikio kuzungumzia suala hilo.

Katika siku za hivi karibuni uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeonekana kusuasua na hata viongozi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakidaiwa kukwepana katika hafla mbalimbali zinazohusu nchi zao pamoja na zile za jumuiya ya Africa mashariki(EAC).

Wiki mbili zilizopita, Rais kagame alikacha kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na zanzibar zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marais wote wanachama wa ( EAC).

Mbali na Kagame kutokuhudhuria maadhimisho hayo, pia aliukacha mkutano wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, lakini alikwenda nchini Kenyana kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaounganishwa na mradi unaoitwa ‘Northern Corridor Infrastructure Project’. Waziri Mkuu Pinda aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.


Source: Gurudumu la Habari