|
Kaburi la marehemu Benadetha Steven aliyefariki dunia hivi karibuni kutokana
na uvimbe tumboni aliyekuwa mkazi wa Mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala
katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga aliyezikwa na kifaranga
cha kuku tumboni na ndugu zake kwa madai kuwa wanaondoa mikosi katika
familia.Pichani ni kaburi lake likiwa limefukuliwa na watu
wasiojulikana-Picha na Kadama Malunde
|
Kaburi la marehemu Benadetha limekutwa limefukuliwa huku sanda na jeneza likiwa linaonekana na alama za nyayo
za miguu ya watu na miguu ya mnyama aina ya fisi zikionekana katika
kaburi hilo.Inasemekana kuna watu walionekana eneo la makaburi juzi
wakiwa na gari na inadaiwa udongo umepelea pengine umechukuliwa-Picha na Kadama Malunde
Wananchi wakiwa kaburini ambapo walisikika wakisema :“Tunalaani kitendo hiki,tumekuta jeneza na sanda
ya marehemu inaonekana,tukaita polisi,hiki kitendo kimefanywa na
binadamu tu maana kaburi lilikuwa refu sana,fisi hawezi kufukua,hapa
kuna miguu ya watu na fisi,fisi nadhani alisikia harufu ya maiti,na fisi
hawezi kuingia kwenye shimo,binadamu wamekosa utu”-Picha na Kadama Malunde
|
Wananchi wakiwa katika eneo la kaburi la marehemu kabla ya kuzika tena-Picha na Kadama Malunde |
|
Mkuu wa upelelezi jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Musa Athuman Taibu(mwenye suti) akiwa kwenye kaburi la marehemu ambapo alisema
jeshi la polisi halina mamlaka ya kufukua kaburi la marehemu bali
mahakama pekee ndiyo yenye yenye mamlaka ya kutoa kibali cha kaburi
kufukuliwa hivyo kuwaomba wananchi kufukia kaburi hilo badala ya
kulifukua.
Benadetha
Steven(35) alikuwa anaishi mtaa wa Mapinduzi kata ya Ndala,alifariki
dunia Januari 1,2015,wakati akitibiwa uvimbe wa tumboni katika hospitali
ya mkoa wa Shinyanga na kuzikwa katika makaburi ya Masekelo ambapo
mazishi yake yalileta utata baada ya ndugu wa marehemu kutoka mkoani
Mara(Wakurya) kuingia kaburini na kuchana tumbo la marehemu kwa wembe
kisha kuchinja kifaranga cha kuku kwa wembe na kuingiza kuku huyo kwenye
tumbo la marehemu.
Picha na Kadama Malunde |
0 comments:
Post a Comment