TAHARUKI
imeibuka katika majengo ya Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani
Rukwa na kusababisha shughuli za mahakamani hapo, zikiwemo za
kusikilizwa mashauri mbalimbali kusimama kwa muda wa takribani dakika
20.
Mtafaruku
huo ulitokea baada ya askari kupiga risasi hewani mahakamani hapo
wakati wakimsaka mahabusu aliyedaiwa kutoroka katika chumba cha mahabusu
mahakamani hapo na kujificha darini.
Mwandishi
wetu alishuhudia askari polisi wakiwa na bunduki mikononi wakihaha
kumsaka mahabusu huyo ambaye alidaiwa kutoroka kupitia upenyo uliopo
katika chumba cha mahabusi mahakamani hapo.
Mkasa
huo ulianzia saa 5 asubuhi na kudumu kwa dakika 20. Hata hivyo,
mahabusu huyo hakuweza kuonekana licha ya jitihada za baadhi ya polisi
kupanda darini kupitia chumba cha mahakama namba mbili bila ya
mafanikio.
Hekaheka
za kumsaka mahabusu huyo zilianza pale baadhi ya watumishi wa
mahakamani hapo na mahakimu kudai kusikia vishindo kwenye dari ambapo
mara moja mahabusu waliokuwa kwenye chumba mahakamani hapo walihesabiwa.
Katika
chumba hicho walitakiwa wawe mahabusu 10 lakini walipohesabiwa kwa mara
ya kwanza ilibainika kuwa alikuwa amekosekana mmoja ndipo msako mkali
ulipoanza huku askari wakihaha kumsaka darini.
Hata
hivyo walipohesabiwa mara ya pili ilibainika kuwa hesabu yao ilikuwa
imetimu kwamba walikuwa 10 lakini haikubainika nani miongoni mwao
alikuwa ametoroka. Hata mahabusu wenyewe hawakuwa tayari kumtaja.
Habari
za kuaminika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa baada ya watumishi
wa mahakama hiyo wakiwemo askari polisi na mahakama kusikia vishindo vya
miguu darini waliamini ilikuwa ni ya mahabusu anayedaiwa kutoroka
katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita
0 comments:
Post a Comment