Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata), limesema litatangaza mrithi wa Mufti wa Tanzania ndani ya siku saba kuanzia jana.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Katibu mkuu wa Bakwata, Sheikh Suleiman Lolila,
alisema utaratibu unaendelea kuhakikisha katika kipindi hicho jina la
Mufti mpya linapatikana.
Kuchaguliwa
kwa kiongozi huyo mpya wa waumini wa dini ya Kiislam nchini, kunafuatia
kufariki kwa aliyekuwa Sheikh mkuu, Mufti Issa Shabani Bin Simba usiku
wa kuamkia Juni 15 katika Hospitali ya TMJ ya jijini Dare s Salaam.
Mufti
Simba alizikwa siku ya pili yake katika makaburi ya Nguzo nane mjini
Shinyanga, ambapo mazishi yake yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, kidini na vyama vya
siasa.
“Mchakato
wa kumpata Sheikh Mkuu wetu utakamilika ndani ya siku saba kuanzia
sasa, wananchi na waumini wa dini ya kiislam wawe wavumilivu katika
kipindi hiki,” alisema Sheikh Lolila.
Katibu
mkuu huyo hakutaka kuweka wazi sehemu wanapokutana wajumbe wa Baraza la
Ulamaa ambao ndilo lenye mamlaka ya kumchagua kiongozi.
Hata
hivyo, baadhi ya watu wanaotajwa kushika nafasi hiyo ni Kadhi Mkuu,
Sheikh Abdallah Mnyasi na manaibu wake Sheikh Abubakar Zuber na Sheikh
Ali Muhidin Mkoyogile.
Wengine
ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Ferej, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga,
Ismail Makusanya, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa na Kadhi wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Hamid Masoud Jongo.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment