Moses
Mongo ambaye ni Mratibu wa Kanda ya Ziwa kutoka Taasisi ya Umoja wa
Mataifa (UNA-TANZANIA) amesema wanafunzi wa Vyuo Vikuu wanaongoza kwa
utoaji wa mimba kwa njia za kienyeji kwa kutumia mwarobaini na bluu ya
kuweka kwenye nguo nyeupe.
Mongo alisema katika utafiti walioufanya mwaka 2014 katika Vyuo Vikuu vinne Kanda ya Ziwa wamebaini wanafunzi kutoa mimba kienyeji.
“Utafiti
tuliofanya 2014 kwa kuzungumza na wanafunzi kila Chuo au Shule
tumebaini wapo wanafunzi waliotoa mimba na wapo waliofariki kwa kutoa
mimba lakini kwa kificho”—Moses Mongo.
Mongo alisema
katika mazungumzo na wanafunzi hao walieleza kuwa suala la utoaji wa
mimba ni la kawaida na matumizi ya kondomu huwa ni pale wanapoanza
uhusiano kabla ya kuzoeana.
0 comments:
Post a Comment