Serikali
ya China imepiga marufuku wanafunzi, walimu na watumishi wa umma katika
eneo la Xinjiang lenye Waislamu wengi kutekeleza ibada ya Saumu kwenye
mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Serikali pia imezuia watu kuhudhuria
marasimu yoyote ya kidini ikiwa ni pamoja na ibada za usiku. Taarifa ya
serikali imetaka biashara kwenye hoteli na mikahawa kufunguliwa nyakati
za mchana kama kawaida. Wanaharakati wa Kiislamu wamepinga agizo hilo la
serikali wakisema linalenga kuhujumu dini tukufu ya Kiislamu.
Kwa
miaka kadhaa sasa, serikali ya China imekuwa ikitekeleza sheria hiyo ya
kibaguzi, na mwaka uliopita, watu kadhaa walifikishwa kortini kwa
kukaidi sheria hiyo na kutekeleza ibada ya funga. Ingawa serikali
inasema lengo la kuweka sheria hiyo ni kuhakikisha masuala ya dini
hayavurugi muundo wa jamii, duru za kuaminika zinasema sheria hiyo ina
malengo ya kiuchumi kwani imewekwa ili kuhakikisha nguvu kazi ya taifa
haipungui katika mwezi wa Ramadhani.
0 comments:
Post a Comment