Mamlaka ya usafirishaji nchini
Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege ya yanayodaiwa kupatikana
ndani ya Bahari ya Hindi yanachunguzwa ili kubaini kama ni ya ndege ya
Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote kwa muda
mrefusasa.
Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzihao ambao
wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo
ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege.
Hata
hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni mapema mno kutoa uhakika kwamba
mabaki hayo ni lazima yatakuwa ya ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777
ambayo kupotea kwake kumeleta gumzo la kidunia.
Watu wapatao 239 waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo walipoteza maisha.
Akizungumza
mjini New York Marekani, Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia Liow Tiong
Lai amesema nchi yake imetuma wataalamu zaidi kuchunguza mabaki hayo.
"Tunahitaji
kuthibitisha" amekaririwa akisema Waziri Lai,na kusisitiza kuwa kwa
vyovyote vile, mabaki yaliyopatikana yanahitaji kuhakikishwa kabla ya
kuthibitisha zaidi kama ndio hasa mabaki ya MH370.
0 comments:
Post a Comment