WANACHAMA wa Chama cha Wananchi (CUF) wamevamia makao makuu ya
chama hicho leo asubuhi na kusababisha kikao cha mwenyekiti Profesa
Ibrahim Lipumba na wanahabari kuhairishwa.
Mkutano wa
mwenyekiti huyo ulikuwa ufanyike leo saa nne asubuhi makao makuu ya Cuf
yaliyopo Buguruni, Dar es Salaam lakini hadi saa tano, mwenyekiti
alikuwa kwenye kikao cha ndani na “wazee wa chama” waliokuwa wanataka
ufafanuzi kwa baadhi ya mambo.
“Wazee wanataka
ufafanuzi kwa baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na taarifa zilizoenea kuwa
amejiuzulu,” amesema Magdalene Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara
amewaamabia wanahabari.
Hata hivyo, wananchama
waliokuwa nje wakati mwenyekiti Lipumba akiendelea na kikao cha ndani
cha chama hicho walionyesha kushtushwa na taarifa zilizochapishwa kwenye
baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuwa Profesa
Lipumba ameachana na siasa za chama hicho.
Wasiwasi huo
uliongezeka jana mara baada ya mtaalamu huyo wa uchumi kutoonekana
wakati wa kumtangaza Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema, moja
ya chama kinachounda Ukawa huku Juma Duni Haji akipitishwa kama mgombea
mwenza.
0 comments:
Post a Comment