Watalamu
kutoka Ufaransa, Malaysia na Australia wameanza kuchunguza mabaki ya
bawa la ndege iliyopatikana juma lililopita likiwa limesombwa hadi
ufukweni na maji ya bahari Hindi katika kisiwa cha Re-Union karibu na
Madagascar.
Nia hasa ni kubaini iwapo mabawa hayo ni sehemu ya mabaki ya ile ndege ya Malaysia ya MH370, iliyotoweka.
Mabaki hayo yamehifadhiwa katika kambi ya jeshi iliyoko katika mji wa Toulouse.
Wataalamu hao watachukua alama za rangi na alama nyingine yeyote ile itakayowasaidia katika utambuzi wa ndege hiyo.
Sehemu iliyoshikana na ndege pia inachunguzwa ili kujua ilimeguka kutoka wapi.
Ndege hiyo ya MH370, ilitoweka angani mwezi Machi mwaka jana ikiwa na abiria 239 na wahudumu wa ndege.
chanzo: BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment