Mwanariadha Oscar Pistorius.
Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Mwanariadha mahiri wa nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius
anatarajiwa kuachiwa Ijumaa hii baada ya kuonyesha tabia nzuri akiwa
gerezani. Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani mwaka
uliopita kwa kosa la kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp katika usiku wa
Siku ya Wapendanao 'Valentine's Day'.
Wakati akitoa hukumu ya staa huyo, Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa
kiongozi wa mashtaka nchini Afrika Kusini alishindwa kuthibitisha kuwa
Pistorius alikusudia kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp alipompiga
risasi nyumbani kwake akidhani kuwa ni mwizi.
0 comments:
Post a Comment