LATEST POSTS

Monday, September 24, 2012

Mwenge wa uhuru ulipokelewa Wilaya ya Urambo siku ya tarehe 23/09/2012 katika Kijiji cha Izimbili Kata Uyumbu. Mwenge huo ulipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo ukitokea Wilaya ya Sikonge. Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo kuupokea Mwenge huo wa Uhuru, Kiongozi wa mbio za Mwenge Mh. Kapten Mwandosa aliueleza umati wa watu uliokua umejitokeza kuupokea mwenge huo kuwa, kauli mbiu ya mbio za Mwenge mwaka huu ni KUHAMASISHA, KUPAMBANA NA MAADUI WATATU WA MAENDELEO ( HIV/AIDS, Madawa ya kulevya,bangi na gongo na Rushwa.

Kapteni Mwandosa alisema kuwa, mbali ya maadui wakubwa watatu waliotangazwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambao ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, hivi sasa, kuna maadui wengine wa maendeleo ambao ni HIV/AIDS, Madawa ya kulevya, bangi na gongo pamoja na rushwa. Aliwataka Wananchi wapambane na maadui hao wa maendeleo ili kujiletea ustawi wa maisha kwani maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana endapo tu kila mmoja atajituma kufanya kazi kwa bidii.
Mbio hizo za Mwenge zilindua miradi ya maendeleo ipatayo kumi na tatu (13) Wilayani Urambo


Mkuu wa Wilaya ya Urambo Mhe. Anna Magoa akifurahia mapokezi ya Mwenge huko Izimbili

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 
 
 








0 comments: