LATEST POSTS

Friday, June 28, 2013

FAMILIA YA MZEE MANDELA YAVILALAMIKIA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA KWA KUWEKA KAMBI KATIKA HOSPITALI ALIYOLAZWA MZEE MADIBA


Huku hali ya Mheshimiwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mhe.Nelson Mandela ikiripotiwa kuimalika tofauti na ilivyokuwa juzi, Binti mkubwa wa Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini Bi. Makaziwe Mandela amevilalamikia vyombo vya habari vya Kimataifa kwa kudai kwamba vinaingilia uhuru na usiri wa MzeeMandela.
 
Bi Makziwe alisema kuwa, kwa vyombo vya habari kuweka kambi katika hospitali aliyolazwa baba yakeni kuingilia usiri na kuvuka mipaka.
Bi Makeziwe alitoa malalamiko hayo huku akiilinganisha hali hiyo na hali ya aliyekuwa Waziri Mkuu waUingereza Bi Margareth Thatcher alipokuwa akiumwa na kulazwa hospitalini. Alisema, Bi. Margareth Thatcher alipokuwa akiumwa, hakuona vyombo vya habari vya Kimataifa vikifanya kama vinavyofanya sasa kwa baba yake hivyo anakichukulia kitendo hicho nikitendo kuwa na chembechembe za kibaguzi.
" Au ni kwa sababu sisi ni Waafrika hivyo watu hawawezi kuheshimu sheria yoyote ya Nchi hii? Hikini kitu kibaya sana".
 
Katika kujibu malalamiko hayo, vyombo vya habari vilijitetea kwakusema kuwa, vipo katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuujulisha ulimwengu hali ya afya ya Rais huyo wa zamaniwa Afrika Kusini inavyoendelea kwakuwa Mzee huyo ni mtu muhimu sana kwa Taifa lake na ulimwengu kwa ujumla.
Mzee Mandela amelazwa katika hospitali ya Pretoria tangu june 8,2013.
 
 
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mheshimiwa Nelson Mandela
 
Binti Mkubwa wa Mheshimiwa Nelson Mandela Bi Makaziwe Mandela.
 
Vyombo vya habari vya Kimataifa kama vinavyoonekana pichani.
 
 

0 comments: