LATEST POSTS

Saturday, June 29, 2013

WAJUMBE WA BARAZA LA KATIBA WILAYANI URAMBO WAPEWA RASIMU YA KATIBA


Wajumbe wa Baraza la KatibaWilaya la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo waligawiwa Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Abel Sengerema ili Wajumbe hao waweze kwenda kuisoma na kuipitia kwa kina na kubaini mapungufu yaliyomo ndani ya Rasimu hiyo na kutoa mapendekezo na maoni yao ya nini kifanyike ili kuiboresha Rasimu hiyo na kwamba mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye vikao vya ngazi za juu vinavyofuata.
Aidha, Mwanasheria hiyo aliwapongeza Wajumbe hao wa Baraza la Katiba Wilaya kwa kuchaguliwa kuwa Wajumbe wa Baraza la Katiba Wilaya.
Aidha, aliwaeleza Wajumbe kuwa, wao kama Wajumbe wa Baraza hilo, kazi yao kubwa nikuwawakilisha Wananchi waliowachagua katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


 
Wajumbe wa Baraza la Katiba Wilaya ya Urambo wakimsikiliza Mwanasheria wa Halmashauri hiyo wakati akiwapa maelekezo ya namna ya kuisoma Rasimu ya Katiba mpya na kutoa maoni na mapendekezo yao juu ya Rasimu hiyo.

 
Bw.Abel Sengerema Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo akiongea na Wajumbe wa Baraza la Katiba Wilaya.

 
 
Bw. Sengerema akiwaonyesha Wajumbe Rasimu ya Katiba Mpya

 
Wajumbe wapo makini kumsikiliza Mratibu wa Baraza la Katiba



 
Wajumbe wakiingaliaRasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania





 


 




 
 

0 comments: